Rudi

Kiswahili

سواحيلي

Masomo Muhimu

1 video
PDF

Uoshaji

3 video
Description of Wudu
0:00 / 0:00
How to Perform Wudu
0:00 / 0:00
Wudu Affairs
0:00 / 0:00

Sala

3 video
Description of Prayer
0:00 / 0:00
Salah with Duaa
0:00 / 0:00
How to Perform Prayer
0:00 / 0:00

Maswali Muhimu

272 maswali
Kitengo cha ibada:42

Swali: 1- Nani Mola wako?

Jawabu: Mola wangu ni Mwenyezi Mungu aliyenilea na akalea watu wote kwa neema zake.
Na ushahidi ni kauli yake Mtukufu:
"Shukurani zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu mola wa viumbe vyote" [Suratul Fatiha: 2]

Swali: 2- Ni ipi dini yako?

Jawabu: Dini yangu ni uislamu: Nao Ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa kumpwekesha, na kunyenyekea kwa kumtii, na kujiepusha na ushirikina pamoja na washirikina.
Amesema Allah Mtukufu:
"Hakika dini inayo kubaliwa kwa Mwenyezi Mungu ni Uislamu" [Surat Al Imran: 19]

Swali: 3- Nani Nabii wako?

Jawabu: Ni Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake.
Amesema Allah Mtukufu:
"Muhamadi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu" [Surat Al-fath :29]

Swali: 4- Taja neno la Tauhidi, na ni ipi maana yake?

Jawabu: Neno la Tauhidi ni "Laa ilaaha illa llaahu" Na maana yake: Ni kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Basi tambua ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu" [Suratu Muhammad: 19]

Swali: 5- Yuko wapi Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka?

Jawabu: Mwenyezi Mungu yuko mbinguni juu ya Arshi, yuko juu ya viumbe vyote, Amesema Mtukufu: "Mwingi wa rehema, juu ya 'Arsh Amelingana, yaani Amekuwa juu na Ameangatika, kulingana kunakonasibiana na utukufu Wake na ukubwa Wake." [Suratu Twaha: 5] Na alisema: "Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, Ndiye Mwenye kutenza nguvu, Aliye juu ya waja Wake. Shingo zimemdhalilikia na majabari wamenyongeka Kwake. Yeye Ndiye Mwenye hekima Anayeweka vitu mahali pake kulingana na hekima Yake. Ndiye Mtambuzi Ambaye hakuna kitu chenye kufichikana Kwake". [Suratul An'am: 18].

Swali: 6- Nini Maana ya kushuhudia kuwa Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu?

Jawabu: Maana yake: Ni kuwa Mwenyezi Mungu kamtuma kwa walimwengu wote ili awape habari njema na awaonye.
Na ni wajibu:

1- Kumtii katika yale aliyoyaamrisha.
2- Kumsadikisha katika yale aliyoyaeleza.
3- Kutomuasi.
4- Asiabudiwe Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yale aliyoyafundisha kama sheria, nako ni kuiga kupitia mafundisho yake (Sunna) na kuacha uzushi.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Mwenye kumtii Mtume basi hakika atakuwa kamtii Mwenyezi Mungu" [Suratun Nisaa: 80], na akasema Mtukufu "Na hatamki kwa matamanio 3- Bali huo ni ufunuo anafunuliwa" [Surat Najm: 3,4]. Na anasema aliyetakasika na kutukuka: {Hakika nyinyi mna kiigizo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu na kumtaja kwa wingi} ((21)), [Suratul Israi: 21].

Swali: 7- Kwanini alituumba Mwenyezi Mungu?

Jawabu: Alituumba kwa ajili ya kumuabu yeye pekee asiye na mshirika.
Si kwa ajili ya upuuzi wala mchezo.
Amesema Allah Mtukufu:
{Sikuumba majini wala watu ila ni kwa lengo la kuniabudu} (56), [Suratu Dhariyat: 56].

Swali: 8-Ni ipi maana ya Ibada?

Jawabu: Ni jina linalokusanya yale yote anayoyapenda Mwenyezi Mungu na kuyaridhia katika maneno na matendo ya siri na ya wazi.
Matendo ya wazi:
Mfano kama kumtaja Mwenyezi Mungu kwa ulimi, miongoni mwa tasbihi (kusema Sub-haanallaah) na tahmidi (kusema Alhamdulillaah) na takbiri (kusema Allaahu Akbar) na swala na Hijja.
Matendo ya siri:
Mfano kama kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuwa na hofu na matumaini.

Swali: 9- Ni wajibu upi mkubwa juu yetu?

Jawabu: Wajibu mkubwa kwetu sisi: Ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Swali: 10- Ni zipi aina za Tauhidi?

Jawabu: 1- Tauhidur rubuubiya (Tauhidi ya ulezi) Nayo ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji, mgawa riziki Mmiliki na mpangiliaji, yeye pekee asiye na mshirika wake.
2- Tauhidul uluuhiyya (Tauhidi ya uungu): Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ibada, asiabudiwe yeyote ila Mwenyezi Mungu Mtukufu.
3- Tauhidul Asmaai wasswifaati (Tauhidi ya majina na sifa): Nayo ni kuyaamini majina na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu zilizokuja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, bila kupiga mfano wala kushabihisha wala kupotosha.
Na ushahidi wa aina hizi tatu za tauhidi:
Ni kauli yake Mtukufu: «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake, Ndiye Mmiliki, Muumba na Mwendeshaji wa hivyo vyote, basi muabudu Yeye Peke Yake, ewe Nabii, na uvumilie katika kumtii, wewe na waliokufuata, Hana mfano Wake kitu chochote katika dhati Yake, sifa Zake na vitendo Vyake.» [Suratu Mariam: 65].

Swali: 11- Ni ipi dhambi kubwa?

Jawabu: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kitu kingine.
Amesema Allah Mtukufu:
"Hakika Mwenyezi Mungu, Hamsamehi aliyemshirikisha Yeye na yeyote miongoni mwa viumbe Wake au akamkufuru kwa aina yoyote ya ukafiri mkubwa. Lakini Anayasamehe na kuyafuta madhambi yaliyo chini ya ushirikina kwa Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na yeyote anayemshirikisha Mwenyezi Mungu na mwingine, hakika amefanya dhambi kubwa. [Suratun Nisaa: 48]

Swali: 12- Taja ushirikina na aina zake.

Jawabu: Ushirikina: Ni kuielekeza aina yoyote miongoni mwa aina za ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Aina zake:

Shirki kubwa; Mfano: Kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kumsujudia asiyekuwa yeye Mtakasifu, au kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Shirki ndogo; Mfano:
Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au mahirizi, nayo ni yale yanayotundikwa kwa ajili ya kuleta manufaa au kuzuia madhara, na shirki ndogo kabisa ni kujionyesha, mfano kama mtu kupendezesha swala yake kwa kuwa anaona kuna watu wanamtazama.

Swali: 13- Je! kuna yeyote anayejua ghaibu (mambo yaliyofichikana) zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu?

Jawabu: Hakuna ajuaye ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee,
Alisema Allah Mtukufu:
"Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Hakuna yeyote ajuaye, mbinguni wala ardhini, jambo lolote lililofichikana ambalo Mwenyezi Mungu Amejihusisha Mwenyewe kulijua. Na wao hawajui ni lini watafufuliwa kutoka makaburini mwao wakati wa Kiyama kusimama.» [Suratun Namli: 65]

Swali: 14- Idadi ya nguzo za imani.

Jawabu: 1- Kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu.
2- Na Malaika wake.
3- Na vitabu vyake.
4- Na Mitume wake.
5- Na siku ya mwisho.
6- Na makadirio kheri yake na shari yake.
Na ushahidi:
Ni hadithi ya Jibrili ambayo ni mashuhuri iko katika sahihi Muslim, alisema Jibrili kumwambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake. "Basi nieleze kuhusu imani, akasema: Ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho na kuamini makadirio kheri yake na shari yake."

Swali: 15- Fafanua nguzo za imani.

Jawabu: Kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ni kumuamini Mwenyezi Mungu kuwa yeye ndiye aliyekuumba na akakuruzuku, na yeye ndiye Mfalme na mpangiliaji peke yake wa viumbe vyote.
Naye ndiye muabudiwa, hakuna muabudiwa kwa haki zaidi yake.
Na kuwa yeye ni Mtukufu Mkuu aliye kamilika Mwenye sifa zote, na ana majina mazuri mno na sifa za hali ya juu, hana mshirika, na hakimfanani chochote Mtukufu.
Kuamini Malaika:

Nao ni viumbe kawaumba Mwenyezi Mungu kwa Nuru, na kwa ajili ya kumuabudu yeye na kwa ajili ya utiifu mkamilifu katika amri zake.
-Miongoni mwao ni Jibrili Amani iwe juu yake anayeteremka na ufunuo (Wahyi) kwa Manabii.
Kuamini vitabu:

Navyo ni vitabu alivyo viteremsha Allah juu Mitume wake.
Kama Qur'ani:
Kwa Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake.
-Injili: kwa Issa- Amani iwe juu yake.
-Taurati: kwa Mussa- Amani iwe juu yake.
-Zaburi: kwa Daudi- Amani iwe juu yake.
-Nyaraka za Ibrahim Amani iwe juu yao: Ibrahim na Mussa.
Kuamini mitume:

Nao ni wale aliowatuma Mwenyezi Mungu kwa waja wake ili wawafundishe, na wawabashirie mazuri na pepo, na wawaonye dhidi ya shari na moto.
-Na wabora wao ni wenye uthubutu, (ulul a'zmi) Nao ni:
Nuhu Amani iwe juu yake.
Ibrahim Amani iwe juu yake.
Mussa Amani iwe juu yake.
Issa Amani iwe juu yake.
Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake.
Kuamini siku ya mwisho:

Nayo ni yale yatakayo kuwa baada ya kifo katika makaburi, na siku ya kiyama, na siku ya kufufuliwa na kuhesabiwa, kiasi ambacho watatulizana watu wa peponi katika makazi yao, na watu motoni katika makazi yao.
Kuamini Makadirio kheri yake na shari yake.
Makadirio:
Ni kuitakidi kuwa Mwenyezi Mungu anajua kila kitu kinachotokea katika ulimwengu, na kuwa yeye alikiandika katika ubao uliohifadhiwa, na akataka kutokea kwake na kukiumba kwake.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Hakika sisi kila kitu tumekiumba kwa makadirio". [Suratul Qamar: 49].
Nayo yako katika daraja nne:

Daraja ya kwanza: Ni Elimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na miongoni mwake ni elimu yake iliyokitangulia kila kitu, kabla ya kutokea kwa vitu na baada ya kutokea kwake.
Na ushahidi wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Hakika Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Anajua ni lini Kiyama kitasimama. Na Yeye Ndiye Anayeteremsha mvua kutoka mawinguni, hakuna awezaye hilo yeyote isipokuwa Yeye. Na Anajua vilivyomo ndani ya vizazi vya wanawake. Na Anajua kitakachotendwa na kila mtu wakati ujao. Na hakuna nafsi inayojua itafia wapi. Ni Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake Ndiye Anayehusika kwa kujua hayo yote. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtambuzi, Ameyazunguka mambo ya nje na ya ndani, hakuna chochote katika hayo kinachofichikana Kwake." [Suratu Luqman: 34].
Daraja ya pili:
Nikuwa Mwenyezi Mungu aliandika hilo katika ubao uliohifadhiwa, kila kitu kilichotokea na kitakachotokea basi kimeandikwa kwake katika kitabu.
Na ushahidi wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilichoko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila vyote hivyo vimo katika Kitabu kinacho bainisha} (59), [Suratul An'am: 59].
Daraja ya tatu:
Nayo ni kuwa kila kitu kinatokea kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na wala hakitokei kitu kwake wala kwa viumbe wake isipokuwa ni kwa matakwa yake Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na ushahidi wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Atakayetaka miongoni mwenu anyooke katika njia. (28) na wala hamuwezi kutaka nyinyi isipokuwa atake Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu wote (29)" [Suratut takwiri: 28,29]
Daraja ya nne: Ni kuamini kuwa kila kilichopo kimeumbwa, alikiumba Mwenyezi Mungu, na aliumba dhati yake na sifa zake na harakati zake, na kila kitu kinachoambatana nacho.
Na ushahidi wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni na hayo mnayoyafanya. (96)" [Suratu Swafat: 96].

Swali: 16- Ni nini maana ya Qur'ani?

Jawabu: Ni maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hayajaumbwa.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na pindi yeyote, miongoni mwa washirikina, akiomba kuingia kwenye himaya yako, ewe Mtume, na akataka amani, basi mkubalie maombi yake ili apate kuyasikia maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu na auone uongofu wake," [Suratu Tauba: 6].

Swali: 17- Sunna ni nini?

Jawabu: Ni kila kauli au kitendo au kukiri kwake Mtume au sifa ya kimaumbile au kitabia ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.

Swali: 18- Uzushi ni nini? na je tuukubali?

Jawabu: Ni kila walichokizua watu katika dini, na wala hakikuwepo katika zama za Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake na maswahaba zake.
*Hapana, hatuukubali na tunaukataa.
Kwa kauli yake Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake:
"Kila uzushi ni upotovu" Imepokelewa na Abuu Daud
Na mfano wake: Ni kuongeza katika ibada, kama kuzidisha katika udhu kuosha mara ya nne, na kama kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume, haya hayakupokelewa kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake na maswahaba zake.

Swali: 19- Taja itikadi ya kupendana kwa ajili ya Allah na kutengana kwa ajili yake.

Jawabu: Kupendana: Ni mapenzi ya waumini na kusaidizana kwao.
Amesema Allah Mtukufu:
{Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki}. [Suratu Tauba: 71].
Na kutengana kwa ajili ya Allah:
Ni kuwachukia makafiri na kuwafanyia uadui.
Amesema Allah Mtukufu:
"Hakika imekuwa kwenu nyinyi ni kiigizo chema kwa Ibrahim na wale waliopamoja naye, pale waliposema kuwaambia watu wao; 'Hakika sisi tumejitenga mbali na yale mnayoyaabudu kinyume na Mwenyezi Mungu, tumekupingeni na umedhihiri kati yetu sisi na nyinyi uadui na chuki milele mpaka mumuamini Mwenyezi Mungu peke yake" [Suratul Mumtahina: 4]

Swali: 20- Je anakubali Mwenyezi Mungu dini nyingine isiyokuwa uislamu?

Jawabu: Hakubali Mwenyezi Mungu dini isiyokuwa uislamu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na mwenye kuchagua isiyokuwa dini ya kiislamu haitokubaliwa kwake naye Akhera atakuwa ni miongoni mwa waliopata hasara (85)" [Surat Al Imrani: 85]

Swali: 21- Ukafiri unakuwa kwa kauli na matendo na itikadi, taja mfano wa hilo?

Jawabu: Mfano wa kauli: Ni kumtukana Mwenyezi Mungu Mtukufu au Mtume wake Rehema na Amani ziwe juu yake.
Mfano wa matendo:
Ni kuudhalilisha msahafu au kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mfano wa itikadi:
Ni kuitakidi kuwa kuna mwingine anayestahiki kuabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au kuna muumbaji mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Swali: 22- Unafiki ni nini na ni zipi aina zake?

Jawabu:
1- Unafiki mkubwa: Nao ni kuficha ukafiri na kudhihirisha imani.
Na huu unamtoa mtu katika uislamu nao ni katika ukafiri mkubwa.
Amesema Allah Mtukufu:
"Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa motoni na wala hawatompata yeyote wa kuwanusuru" [Suratun Nisaa: 145]
2- Unafiki mdogo:
Kuongopa na kutotimiza ahadi na kufanya hiyana katika amana.
Na huu haumtoi mtu katika uislamu, nao ni katika madhambi na mfanyaji anajitia katika adhabu.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Alama za Mnafiki ni tatu: Anapozungumza husema uongo, na anapoahidi huenda kinyume, na akiaminiwa hufanya hiyana". Ameipokea Bukhari na Muslim.

Swali: Ni nani Mtume wa mwisho na manabii?

Jawabu: Ni Muhammad Rehema na Amani ziwe juu yake.
Amesema Allah Mtukufu:
{Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii} [Suratul Ahzaab: 40]. -Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Na mimi ndiye mwisho wa Manabii hakuna Nabii baada yangu" Imepokelewa na Abuu Daud na Tirmidhiy na wengineo.

Swali: Muujiza ni nini?

Jawabu: Muujiza: Ni kila alichokitoa Mwenyezi Mungu kuwapa manabii wake katika mambo ambayo yako nje ya mazoea ya kawaida, ili kuonyesha ukweli wao, mfano:
-Kupasuka mwezi kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.
-N kupasuka kwa Bahari kwa Mussa Amani iwe juu yake, na kuangamizwa Firauni na majeshi yake.

Swali: 25- Maswahaba ni akina nani? na je niwapende?

Jawabu: Ni yule aliyekutana na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akamuamini na akafa katika uislamu.
-Ndiyo tunawapenda na tunaiga kutoka kwao, nao ni wabora kuliko watu wengine baada ya manabii.
Na wabora wao zaidi ni:
Makhalifa (viongozi) wanne:
Abuu bakari Radhi za Allah ziwe juu yake
Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake-
Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake-
Ally -Radhi za Allah ziwe juu yake-

Swali: 26- Ni akina nani mama wa waumini?

Jawabu: Hao ni wake za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-.
Amesema Allah Mtukufu:
"Nabii ni bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao, na wake zake ni mama zao". [Suratul Ahzab: 6].

Swali: 27- Ni zipi haki za watu wa familia ya nyumba ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwetu sisi?

Jawabu: Tunawapenda na tunawajali, na tunamchukia mwenye kuwachukia, na wala hatuchupi mipaka kwao, nao ni wake zake na watoto wake na ukoo wa bani Hashim na bani Abdul Muttwalib katika waumini.

Swali: 28- Ni upi wajibu wetu mbele ya wasimamizi wa mambo ya waislamu?

Jawabu: Wajibu wetu: Ni kuwaheshimu na kusikiliza na kuwatii katika mambo ambayo si maasi, na kutojitoa katika uongozi wao kwa kuwapinga, na kuwaombea dua na kuwapa nasaha kwa siri.

Swali: 29- Ni ipi nyumba ya waumini?

Jawabu: Ni pepo, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu Atawatia, wale ambao waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakajikita katika Imani hiyo na wakafanya mema, kwenye mabustani ya Pepo ambayo inapita mito chini ya majumba yake ya kifahari na miti yake." [Suratu Muhammad: 12]

Swali: 30- Ni ipi nyumba ya makafiri?

Jawabu: Ni moto, Amesema Allah Mtukufu: "Basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe umeandaliwa kwa ajili ya makafiri" [Suratul Baqara: 24].

Swali: 31- Hofu ni nini? Na je kutaraji ni nini? Na ni upi ushahidi?

Jawabu: Hofu: Ni kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuogopa adhabu zake.
Kutaraji:
Ni kutaraji thawabu za Mwenyezi Mungu na msamaha wake na rehema zake.
Na ushahidi ni kauli yake Allah Mtukufu:
"Hao washirikina wanawaomba, miongoni mwa Manabii, watu wema na Malaika, wao wenyewe wanashindana kujiweka karibu na Mola wao kwa matendo mema wanayoyaweza, wanatarajia rehema Yake na wanaogopa adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako ndiyo ambayo inatakikana kwa waja wawe na tahadhari nayo na waiogope(adhabu ya moto)". [Suratul Israai: 57]. Na amesema Allah Mtukufu: {Wape habari, ewe Mtume, waja wangu kwamba mimi ni mwenye kuwasamehe Waumini wenye kutubia, ni mwenye huruma kwao 49 Na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iumizayo}. [Suratul Hijri: 49,50].

Swali 32: Taja baadhi ya majina na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Jawabu: Allah, Arrabbu (Mola/Mlezi), Assamiiu (Msikivu), Albaswiru (Mwingi wa kuona), Al'aliimu (Mjuzi), Alrazzaq (Mgawa riziki), Al Hayyu (Aliye hai), Al A'adhwiimu (Mtukufu) Na mengineyo katika majina mazuri na sifa za hali ya juu.

Swali: 33- Fafanua majina haya?

Jawabu: Allah: maana yake ni Mola muabudiwa wa kweli, yeye pekee asiye na mshirika wake.
Arrabbu (Bwana): Yaani: Muumba na mmiliki mgawa riziki na mpangiliaji yeye peke yake aliyetukuka.
Assamiiu:
Ambaye usikivu wake umekienea kila kitu, na anazisikia sauti zote pamoja na kutofautiana kwake na kuwa na aina mbali mbali.
Albaswiru:
Anaye kiona kila kitu, na anakiona kila kitu kiwe kidogo au kikubwa.
Al A'liimu:
Naye ni yule ambaye elimu yake imekizunguka kila kitu kilichopita na kilichopo na kijacho.
Alrahman:
Ambaye huruma yake imekienea kila kiumbe na kila kilicho hai, waja wote na viumbe vyote viko chini ya huruma yake.
Arrazzaaq:
Ambaye anajukumu la kugawa riziki kwa viumbe wote kuanzia watu na majini na wanyama wote.
Al hayyu:
Aliye hai ambaye hafi, na viumbe wote wanakufa.
Al A'dhwiim:
Mwenye ukamilifu wote na utukufu wote katika majina yake na sifa zake na vitendo vyake.

Swali: 34- Ni upi wajibu wetu mbele ya wanachuoni wa waislamu?

Jawabu: Tunatakiwa kuwapenda na kurejea kwao katika maswala mbali mbali na yale yanayotokea katika mambo ya sheria, na hatuwasemi ila kwa mazuri, na mwenye kuwataja kwa mambo tofauti na hayo katika mambo mabaya; basi huyu atakuwa hayuko katika njia sahihi.
Amesema Allah Mtukufu:
"Mwenyezi Mungu Anawapandisha vyeo wale Waumini miongoni mwenu, na Anawapandisha vyeo wale wenye elimu daraja nyingi kwa kuwapatia malipo mema na daraja za kupata radhi. Na Mwenyezi Mungu Anayatambua matendo yenu, hakuna chochote kinachofichikana Kwake katika hayo, na Yeye ni mwenye kuwalipa nyinyi kwayo" {Suratul Mujadila: 11].

Swali: 35- Ni akina nani vipenzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu? (Mawalii).

Jawabu: Ni waumini wachamungu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Tambueni kuwa vipenzi wa Mwenyezi Mungu hawatokuwa na hofu juu yao na wala hawatohuzunika, (62) Wale walioamini na wakawa wachamungu" [Suratu Yunus: 62,63].

Swali: Je Imani ni kauli na matendo?

Jawabu: Imani ni kauli na matendo na itikadi.

Jawabu: je Imani inaongezeka na kupungua?

Jawabu: Imani inaongezeka kwa kumtii Mwenyezi Mungu na inapungua kwa kufanya maasi.
Amesema Allah Mtukufu:
"Hakika wenye kumuamini Mwenyezi Mungu ni wale ambao akitajwa Mwenyezi Mungu hulainika nyoyo zao na wasomewapo aya za Mwenyezi Mungu zinawazidishia Imani na kwa Mola wao wanategemea" [surat Anfaal:2]

Swali: 38- Ihsani (wema) Ni nini?

Jawabu: Ni Kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona na ikiwa humuoni basi Yeye anakuona.

Swali: 39- Ni wakati gani matendo yanakuwa yamekubalika kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na ?

Jawabu: kwa sharti mbili:
1- Yatakapokuwa halisi kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
2- Na yatakapokuwa katika mafundisho ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.

Swali: 40- Ni kupi kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu?

Jawabu: Ni kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa na kuondoa madhara, pamoja na kuchukua sababu.
Amesema Mwenyezi mungu Mtukufu:
"Na mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi yeye humtosheleza" [Suratu Twalaq: 3.]
Humtosheleza: Yaani: Humtekelezea kila kitu.

Swali: 41- Ni upi wajibu wa kuamrisha matendo mema na kukataza mabaya?

Jawabu: Kuamrisha mema: Ni kuamrisha katika kila ambalo ni la kumtii Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na uovu: Ni kukataza kila maasi ya kumuasi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Amesema Allah Mtukufu:
"Nyinyi, enyi umma wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni umma bora na ni watu wenye manufaa zaidi kwa watu, mnaamrisha mema, nayo ni yale yanayofahamika uzuri wake kisheria na kiakili, na mnakataza maovu , nayo ni yale yanayoeleweka ubaya wake kisheria na kiakili, na mnamuamini Mwenyezi Mungu kikweli-kweli imani inayotiliwa nguvu na vitendo." [Surat Al Imran: 110]

Swali: 42- Ni akina nani Ahlussunati Wal Jama'a?

Jawabu: Ni wale watakaokuwa katika mfano wa yale aliyokuwa nayo Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake na maswahaba zake katika kauli na matendo na itikadi.
Na wameitwa kuwa ni Ahlussunna:
kwa kufuata kwao mafundisho ya Nabii Rehema na Amani ziwe juu yake, na kuacha kuzua.
Na Jama'a:
(Wamoja) Kwa sababu wao walikubaliana katika haki na wala hawakufarakani.

SEHEMU YA SHERIA.47

Swali: 1- Eleza maana ya Twahara?

Jawabu: Twahara: Ni kuondoa uchafu usioonekana, na kuondoka kwa uchafu.
Kusafisha uchafu:
Nako ni muislamu kuondoa yaliyodondoka katika najisi katika mwili wake, au juu thawabu zake, na katika eneo au mahalali panaposwaliwa hapo.
Twahara ya hadathi:
Nao ni usafi unaokuwa kwa udhu au kuoga, kwa maji masafi, au kutayammamu kwa atakayekosa maji, au akawa na dharura ya kutotumia maji.

Swali: 2- Ni vipi utasafisha kilichopatwa na najisi?

Jawabu: Kwa kukiosha kwa maji mpaka kisafishike.
-Na ama alichokilamba mbwa; kitaoshwa mara saba mara moja kwa udongo.

Swali: 3- Ni upi ubora wa udhu?

Jawabu: Amesema Mtume Sala na amani ziwe juu yake: "pindi muislamu au muumini atakapo tawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayo tokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono kutokana na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka mwislamu anabaki msafi hana madhambi". Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 4- Unatawadha vipi?

Jawabu: Utaosha viganja vya mikono mara tatu.
Na utasukutua na kupandisha maji puani na kuyapenga mara tatu.
Na kusukutua:
Ni kuweka maji mdomoni na kuyazungusha na kuyatema.
Na kupandisha maji:
Ni kuvuta maji kwa pumzi kuyapandisha ndani ya pua kwa mkono wa kulia.
Na kuyapenga:
Nako ni kuyatoa maji puani baada ya kuyapandisha upande wa kushoto.
Kisha kuosha uso mara tatu.
Kisha Kuosha mikono miwili pamoja na viwiko viwili mara tatu.
Kisha kufuta kichwa utaanza mbele ya kichwa kisha utarudisha mikono yako nyuma, na utafuta masikio mawili.
Kisha utaosha miguu yako miwili mpaka katika kongo mbili mara tatu.
Huu ndio ukamilifu, na limethibiti hilo kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake katika hadithi nyingi zilizoko katika Bukhari na Muslim, kazipokea kutoka kwake Othman na Abdallah bin Zaidi na wengineo, Na imethibiti pia kutoka kwake katika kitabu cha Bukhari na wengineo: "Ya kwamba yeye kuna wakati alitawadha mara moja moja, na wakati mwingine alitawadha mara mbili mbili" Yaani: Nikuwa alikuwa akiosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara moja, au mara mbili.

Swali: Ni zipi faradhi za udhu, na ni ipi idadi yake?

Jawabu: Ni zile ambazo hausihi au haukamiliki udhu wa muislamu atakapoacha moja kati yake.
1- Kuosha uso ikiwa ni pamoja na kusukutua na kupandisha maji puani.
2- Kuosha mikono miwili mpaka katika viwiko viwili.
3- Kufuta kicha pamoja na masikio mawili.
4- Kuosha miguu miwili mpaka katika kongo mbili.
5- Kupangilia kati ya viungo, aoshe uso, kisha mikono miwili, kisha afute kichwa, kisha aoshe miguu miwili.
6- Kufululiza: Nako ni kushika udhu kwa muda wa kufuatana, bila kutenganisha nyakati mpaka maji yakauke katika viungo.
- Kama mtu kutawadha nusu ya udhu, kisha aache aje kuukamilisha katika wakati mwingine, udhu wake hausihi (haukubaliki)

Swali: 6- Ni zipi sunna za udhu, na ni ipi idadi yake?

Jawabu: Sunna za udhu: ni zile ambazo kama mtu atazifanya basi atapata ziada ya malipo na thawabu, na kama akiziacha hana dhambi, na udhu wake utakuwa sahihi.
1- Kusema: Bismillaahi.
2- Kupiga mswaki.
3- Kuosha viganga viwili.
4- Kuachanisha vidole.
5- kuosha kwa mara ya pili na ya tatu katika viungo.
6- Kuanzia kulia.
7- Dua baada ya udhu: "Nina shuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika, na nina shuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na ni mtume wake".
8- Swala ya rakaa mbili baada ya udhu.

Swali: 7- Ni ipi idadi ya vitenguzi vya udhu.?

Jawabu: Ni kile kinachotoka katika njia mbili, ya mbele na ya nyuma, kama haja ndogo au kubwa au upepo.
Kulala, au wendawazimu au kuzimia.
kula nyama ya Ngamia.
Kugusa utupu wa mbele au wa nyuma bila kizuizi.

Swali: 8- Tayammamu ni nini?

Jawabu: Tayammamu ni kutumia udongo au kinginecho katika udongo wa ardhi, wakati wa kukosa maji, au dharura ya kutotumia maji.

Swali: 9- Unatayammamu vipi?

Jawabu: Ni kupiga udongo mpigo mmoja kwa viganja viwili, na kufuta uso na juu ya viganja viwili mara moja.

Swali: 10- Ni vipi vitenguzi vya tayammamu?

Jawabu: Ni vitenguzi vyote vya udhu.
ziada ya hapo, ni yatakapopatikana maji.

Swali: 11- Khofu mbili ni zipi, na soksi mbili ni zipi? na je inaruhusiwa kufuta juu yake?

Jawabu: Khofu mbili: Ni viatu vinavyovaliwa mguuni vilivyotokana na ngozi.
Soksi mbili:
Ni vitu vinavyo valiwa mguuni ambavyo si vya ngozi.
Ni sheria kufuta juu yake badala ya kuosha miguu miwili.

Swali: 12- Eleza hekima ya kufuta juu ya khofu mbili?

Jawabu: Ni wepesi na kuondoa uzito kwa waja, hasa hasa nyakati za baridi, na masika na safarini, kiasi ambacho inakuwa tabu kuvua vilivyoko miguuni.

Swali: 13- Ni zipi sharti za kufaa kufuta juu ya khofu mbili?

Jawabu: 1- Awe amezivaa akiwa na twahara, yaani baada ya udhu.
2- Khofu ziwe safi (Twahara) haifai kufuta juu ya najisi.
3- Khofu ziwe zinafunika mahala palazima kuoshwa kwake katika udhu.
4- Kufuta kuwe ndani ya muda maalumu uliowekwa, mkazi ambaye si msafiri: afute ndani ya mchana na usiku wake, na kwa msafiri: ni siku tatu usiku na mchana wake (Masaa 72)

Swali: 14- Ni zipi sifa za kufuta juu ya khofu mbili?

Jawabu: Ama namna ya kufuta ni: aweke vidole vya mikono yake vikiwa vimeloa maji juu ya vidole vya miguu yake kisha anavitembeza mpaka katika muundi wake, atafuta mguu wa kulia kwa mkono wa kulia, na mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto, na ataachanisha vidole vyake na wala asirudie kupitisha, yaani afanye mara moja.

Swali: 15- Ni vipi vinavyotengua kufuta juu ya khofu mbili?

Jawabu: 1- Kumalizika kwa muda wa kufuta, haitakiwi kufuta juu ya khofu baada ya kumalizika kikomo cha muda wa kufuta kisheria, mchana na usiku wake kwa mwenyeji, na michana mitatu na usiku wake kwa msafiri.
2- Kuvua khofu mbili, akivua mtu khofu mbili au moja wapo baada yakuwa amefuta, kufuta juu yake kutakuwa kumebatilika.

Swali: 16- Maana ya swala.

Jawabu: Swala: Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kauli na matendo maalumu, yanayoanza kwa takbiri (Allahu Akbaru) yanayohitimishwa kwa salamu.

Swali: 17- Hukumu ya swala.

Jawabu: Swala ni lazima kwa kila muislamu
Amesema Allah Mtukufu: "Hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa muda maalumu". [Surat Nisaa: 103]

Swali: 18- Ni ipi hukumu ya kuacha swala?

Jawabu: Kuacha swala ni ukafiri, Amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni swala, na atakayeiacha swala basi atakuwa kakufuru" Ameipokea Ahmad na Tirmidhiy na wengineo.

Swali: 19- Ni swala ngapi zinamlazimu muislamu usiku na mchana? na ni ngapi idadi ya rakaa za kila swala?

Jawabu: Ni swala tano mchana na usiku, Swala ya Alfajiri: Rakaa mbili, Na swala ya Adhuhuri: Rakaa nne, Na swala ya Lasiri: Rakaa nne, Na swala ya maghribi: Rakaa tatu, na swala ya Ishaa: Rakaa nne.

Swali: 20- Ni ngapi idadi ya sharti za swala?

Jawabu: 1- Uislamu; haitosihi kwa kafiri.
2- Akili; haikubaliki kwa mwendawazimu.
3- Kupambanua; haikubaliki kwa mtoto mdogo ambaye hajafikia umri wa kupambanua mambo.
4- Nia.
5- kuingia wakati wa swala.
6- Twahara kwa ajili ya kuondoa uchafu (Hadathi).
7- Kujisafisha kutokana na najisi.
8- Kusitiri uchi.
9- Kuelekea kibla.

Swali: 21- Ni ngapi idadi ya nguzo za swala?

Jawabu: Ni nguzo kumi na nne, kama ifuatavyo:
Ya kwanza: Kusimama katika swala za faradhi kwa mwenye kuweza.
Takbira ya kuhirimia swala, nayo ni kusema "Allaahu Akbaru" wakati wa kuanza swala.
Kusoma Suratul Fatiha.
Kurukuu, na atanyoosha mgongo wake uwe sawa sawa na ataweka kichwa chake kiwe sambamba.
Kunyanyuka kutoka katika rukuuu.
Kusimama wima.
Kusujudu, na kuhakikisha paji la uso wake liko chini, na pua yake, na viganja vyake, na magoti yake, na ncha ya vidole vya miguu yake kuwa mahali anaposujudia.
Kunyanyuka kutoka katika sijida.
Kukaa kati ya sijida mbili.
Na sunna:
Ni akae akiwa kaukalia mguu wake wa kushoto na kaunyoosha wa kulia, na auelekeze kibla.
Utulivu, nako ni kutulia katika kila nguzo ya kivitendo.
Tashahudi ya mwisho.
Kukaa kwa ajili ya tashahudi.
Salamu mbili, nako ni mtu kusema mara mbili: "Assalaamu alaikum warahmatullaah".
Kupangilia nguzo -kama tulivyosema-, ikiwa atasujudu kwa mfano kabla ya kurukuu kwa makusudi; swala itabatilika, na kwa kusahau; itamlazimu arudi ili arukuu, kisha asujudu.

Swali 22- Taja wajibu za swala?

Jawabu: Wajibu za swala, nazo ni nane, kama ifuatavyo:
1- Takbira zote isipokuwa takbira ya kuhirimia swala (Ile kuanza swala)
2- Kauli ya: "Samiallaahu liman hamidah" kwa imamu na anayeswali peke yake.
3- Kauli ya: Rabbanaa walakal hamdu".
4- kauli ya: "Sub-haana rabbiyal A'dhwiim" mara moja katika rukuu.
5- kauli ya: "Sub-haana rabbiyal A'laa" mara moja katika sijida.
6- kauli ya: "Rabbighfirli" kati ya sijida mbili.
7- Tahiyatu ya kwanza.
8- kukaa kwa ajili ya tahiyatu ya kwanza.

Swali: 23- Ni zipi sunna za swala?

Jawabu: Ni sunna kumi na moja, kama zifuatazo:
1- Ni kauli ya mswaliji baada ya takbira ya kuhirimia swala: "Sub-haanakallaahumma wabihamdika, watabaaraka smuka, wata'ala jadduka, walaa ilaaha ghairuka" Na hii huitwa dua ya ufunguzi wa swala.
2- kuomba kinga kutokana na shetani aliyelaaniwa.
3- Bismillah.
4- Kauli ya: Aamin.
5- kusoma sura nyingine baada ya suratul Faatiha.
6- Kudhihirisha kisomo kwa imamu.
7- Kauli ya kusema baada ya neno la rukuu (Rabbanaa walakal hamdu) kusema; Mil assamaawaati, wamil al Ardhwi, wamila maa shiita, min shai in ba'd"
8- Kila kinachozidi katika tasbihi ya rukuu: Yaani: kumsabihi Mwenyezi Mungu kwa mara ya pili na ya tatu, na zaidi ya hapo.
9- Kinachozidi zaidi ya mara moja katika tasbihi ya sijida.
10- Kinachozidi zaidi ya mara moja katika kauli kati ya sijida mbili: "Rabbighfirlii".
11- Kuwataki rehema familia ya Mtume Amani iwe juu yao katika tashahudi ya mwisho, na kumuombea baraka yeye na wao, na kuomba dua ya hapo.
Ya nne:
Sunna za vitendo, na huitwa mikao (mionekano):
1- kunyanyua mikono pamoja na takbira ya kuhirimia swala.
2- Na wakati wa kurukuu.
3- Na wakati wa kunyanyuka kutoka katika rukuu.
4- Na kuiachia baada ya hapo.
5- Kuweka mkono wa kulia juu ya kushoto.
6- Kutazama mahali pa kusujudia.
7- Kuachanisha kati ya miguu miwili wakati wa kusimama.
8- Kushika magoti mawili kwa mikono miwili vidole vikiwa vimeachanishwa katika rukuu, na kunyoosha mgongo hapo, na kukifanya kichwa kilingane na mgongo.
9- Kuhakikisha viungo vya kusujudu viko katika ardhi, na viguse mahala pa kusujudia.
10- Kutenganisha kati ya mikono na mbavu, na tumbo lake na mapaja yake, na mapaja yake na miundi yake, na kuiachanisha na magoti, na kusimamisha visigino viwili, na kuweka tumbo za vidole vya miguu miwili katika ardhi vikiwa vimeachanishwa, na mtu aweke mikono yake usawa wa mabega yake ikiwa imekunjuliwa na vidole vikiwa vimefungamanishwa.
11- Kukaa mkao wa kukalia mguu wa kushoto na kusimamisha wa kulia (Iftirashi) katika kikao kati ya sijida mbili, na katika tahiyatu ya kwanza, na kukalia kalio la kushoto na kulaza mguu wa kushoto ndani ya mguu wa kulia (Tawaruku) katika tahiyatu ya pili.
12- Kuweka mikono miwili juu ya mapaja mawili ikiwa imetandazwa, vidole vikiwa vimebananishwa kati ya sijida mbili, na hivyo hivyo katika tahiyatu, isipokuwa katika tahiyatu ataukunja mkono wa kulia kidole kidogo na kinachofuata, na atafanya duara kati ya kidole cha kati na kidole gumba, na ataashiria kwa kidole cha shahada wakati wa kumtaja Mwenyezi Mungu.
13- Mtu kugeuka kulia na kushoto wakati wa kutoa salamu.

Swali: 24- Idadi ya mambo yanayobatilisha swala.

Jawabu: (1) Kuacha nguzo au sharti katika sharti za swala.
(2) Kuzungumza kwa makusudi.
(3) Kula au kunywa.
(4) Harakati nyingi za kufululiza.
(5) Kuacha wajibu miongoni mwa wajibu za swala kwa makusudi.

Swali: 25- Ni namna gani anaswali muislamu?

Jawabu: Namna ya kuswali:
1- Anaelekee kibla kwa mwili wake wote, bila kupinda wala kugeuka geuka.
2- Kisha ananuia swala anayotaka kuiswali, anafanya hivyo moyoni mwake bila kuitamka nia.
3- Kisha atatoa takbira ya kuhirimia swala atasema: (Allahu Akbaru), na atanyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake wakati wa kutoa takbira.
4- Kisha ataweka kiganja cha mkono wake wa kulia juu ya mgongo wa kiganja cha mkono wake wa kushoto, juu ya kifua chake.
5- Kisha atafungua swala na atasema: "Allaahuma baaid bainiy wabaina khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali kati yangu na kati ya makosa yangu) kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi (kama ulivyoweka mbali kati ya mashariki na magharibi, Allaahu naqqiniy min khatwaayaaya (Ewe Mwenyezi Mungu nisafishe kutokana na makosa yangu) kamaa yunaqqath-thaubul abyadh minaddanasi (kama inavyosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu) Allaahummaghsilniy min khatwaayaaya bith-thalji wal maai wal baradi (Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi kutokana na madhambi kwa barafu na maji na baridi".
"(Sub-hanakallahumma wabihamdika,wa tabaarakasmuka ,wa taalajadduka walaa ilaha ghairuka)
-kutakasika ni kwako ewe mola na kushukuriwa ni kwako,limetukuka jina lako,na umetukuka utukufu wako na hakuna mola mwingine zaidi yako-"
6- Kisha ataomba kinga kutokana na shari za shetani, na atasema: "A'udhubillaahi minash-shaitwanir rajiim" Yaani: Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa. 7- Kisha atasoma bismillahi na atasoma suratul fatiha, na atasema: Bismillahir Rahmanir Rahiim (1) "Alhamdulillaahi Rabbil 'aalamiin" Shukurani zote njema anastahiki mola wa viumbe vyote (2). "Arrahmaanir rahiim" Mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu (3) "Maaliki yaumid-diin" Mmiliki wa Siku ya Malipo (4) "Iyyaaka na'budu wa iyyaaka nasta'iin" Wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada (5) . "Ihdinas swiraatwal mustaqiim" Tuongoze katika njia iliyonyooka (6). "Swiraatwalladhiina an 'amta a'laihim, ghairil magh dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" Njia ya wale uliowaneemesha juu yao, na siyo ya wale uliowakasirikia wala ya wale waliopotea (7). [Suratul- Faatiha 1-7]
Kisha anasema: (aaamiin) Yaani: Ewe Mola pokea maombi.
8- Kisha atasoma kiasi anachokiweza katika Qur'ani, na atarefusha kisomo katika swala ya alfajiri.
9- Kisha atarukuu, Yaani: atainamisha mgongo wake kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu, na atatoa takbira wakati wa kurukuu, na atanyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake mawili. Na sunna: anatakiwa anyooshe mgongo wake, na kichwa chake kiwe sawa sawa na mgongo, na ataweka mikono yake juu ya magoti yake mawili akiwa kaachanisha vidole vyake.
10- Na atasema katika rukuu yake: "Sub-haana rabbiyal a'dhwiim" Ametakasika Mola wangu Mtukufu, mara tatu, na kama akiongeza: "Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, Allaahummaghfirlii" basi itakuwa vizuri.
11- Kisha atanyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu akisema: "Sami'allaahu liman hamidah", na wakati huo akinyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake. Na maamuma (anayesalishwa) hatosema: "Sami'allaahu liman hamidah" bali badala yake atasema: "Rabbanaa walakal hamdu" ewe mola wetu sifa njema zote ni zako.
12- Kisha atasema baada ya kunyanyuka kwake: "Rabbanaa walakal hamdu, mil assamaawaati wal ardhwi, wamil amaa shi ita min shai in ba'd"
13- Kisha atasujudu sijida ya kwanza, na atasema wakati wa kusujudu kwake: "Allahu Akbaru", na atasujudu katika viungo vyake saba: Paji la uso na pua, viganja viwili vya mikono, na magoti mawili, na ncha za vidole vya miguu miwili, na atatenganisha kwapa za mikono yake na mbavu zake, na asitandaze mikono yake katika ardhi, na ncha za vidole vyake atazielekeza kibla.
14- Na atasema katika Sijida yake: "Sub-haana rabbiyal a'alaa" Ametakasika Mola wangu aliye juu, mara tatu, na kama akiongeza: "Sub-haanaka llaahumma wabihamdika, Allaahummaghfirlii" basi itakuwa vizuri.
15- kisha atanyanyua kichwa chake kutoka katika sijda huku akisema:"Allahu akbaru".
16- Kisha atakaa kati ya sijda mbili ataukalia mguu wake wa kushoto, na atasimamisha kisigino chake cha kulia, na ataweka mkono wake wa kulia mwisho wa paja lake la kulia karibu na goti, na atakunja vidole viwili, kidole kidogo, na kinachofuata, na atanyanyua kidole cha shahada na atakitikisa wakati wa kuomba kwake dua, na ataweka ncha ya kidole gumba kikiwa sambamba na kidole cha kati kama kimduara hivi, na ataweka mkono wake wa kushoto mwisho wa paja lake la kushoto karibu na goti na vidole vikiwa vimekunjuliwa kuelekea kibla.
17- Na atasema wakati wa kukaa kwake kati ya sijida mbili. "Rabbighfirliiy warahmniiy wahdiniiy warzuquniiy waafiniiy"(Ewe mola wangu nisamehe mimi na unihurumie na uniongoze na uniruzuku na unisamehe)
18- Kisha atasujudu sijida ya pili kama ya kwanza katika yale yanayosemwa na kufanywa, na atatoa takbira wakati wa kusujudu kwake.
19- Kisha atanyanyuka kutoka katika sijida ya pili huku akisema: "Allaahu Akbaru" na ataswali rakaa ya pili kama ya kwanza katika yale yanayosemwa na yanayofanywa, isipokuwa katika rakaa hiyo hatoanza kwa dua ya ufunguzi.
20- Kisha atakaa baada ya kumaliza rakaa ya pili huku akisema: "Allaahu Akbaru", na atakaa kama anavyokaa kati ya sijida mbili hivyo hivyo.
21- Na atasoma tahiyatu katika kikao hiki, na atasema: "Attahiyyaatulillahi,Waswalawaatu watwayyibaatu,Assalaamu Alaika Ayyuha Nabiyyu Wrahmatullahi Wabarakaatuhu, Assalaamu Alaina waalaa ibadillahi swaalihiina, Ash-hadu an-laailaha illa llau wa anna muhamadan rasuulullahi"Allahumma swalli alaa muhammad waalaa ali muhammad, kamaa swalaita alaa ibrahiim waalaa aali ibrahiim Innaka hamiidun majiid,Allahumma Baariki Alaa Muhammad wa alaa aali muhammad ,kamaa baarakta alaa ibraahiim wa- alaa aali ibrahiim innaka hamiidun majiid" Au'dhubillahi min adhabi Jahannam, wami adhabil kabri, wamin fitinatil mahyaa wal mamaati, wamin fitinatila masihid dajjali" Kisha atamuomba mola wake kwa yale anayoyataka katika kheri za dunia na akhera.
22- Kisha atatoa salamu kuliani kwake atasema: "Assalaamu alaikum warahmatullaah" Na kushotoni kwake hivyo hivyo.
23- Na ikiwa ni swala ni ya rakaa tatu au nne; atasimama wakati wa kumalizika kwa tahiyatu ya kwanza, nayo ni: "Ash-hadu an laa ilaaha illa llaahu, wa ash-hadu anna Muhammadan abduhu warasuuluhu".
24- Kisha atasimama wima huku akisema: "Allahu Akbaru", na atanyanyua mikono yake usawa wa mabega yake wakati huo.
25- Kisha atasali kumazia kiasi kilichobakia katika swala yake kwa namna kama ilivyokuwa rakaa ya tatu, isipokuwa hapa ataishia katika kusoma suratul fatiha.
26- Kisha atakaa (tawaruku) yaani: atakalia kalio la kushoto na kusimamisha mguu wa kulia, na atautoa nje mguu wa kushoto kupitia katika muundi wa mguu wa kulia, na ataweka makalio yake katika ardhi, na ataweka mikono yake juu ya mapaja yake kama alivyoiweka katika tahiyatu ya kwanza.
27- Na atasoma katika kikao hiki tahiyatu yote.
28- Kisha atatoa salamu kuliani kwake atasema: "Assalaamu alaikum warahmatullaah" Na kushotoni kwake hivyo hivyo.

Swali: 26- Unasema nini katika nyiradi baada ya salamu ya kumaliza swala?

Jawabu: "Astaghfirullaah" Mara tatu.
"Allahumma antassalaam, waminkassalaam, tabaarakta yaa dhaljalaali wal ikraam".
"Laailaha illa llahu wah'dahu laa shirika lahu ,lahulmulku walahulhamduwhuwa alaa kulli shain qadiir, "Allahuma laa maania limaa aa'twaita walaa muutwiya limaa mana'ata walaa yanfau dhaljaddi minkal jaddu".
"Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul Mulku walahul Hamdu wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun ni'matu walahul Fadhlu, walahuth thanaaul hasan, Laa ilaaha Illa llaahu Mukhliswiina lahud diina walau karihal kaafiruun" Yaani: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, Ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye juu ya kila kitu ni muweza, Hakuna ujanja wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu, Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Na hakuna tunayemuabudu ila yeye, ana neema na ana fadhila, na ana sifa njema, Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu tunamtakasia dini hata kama makafiri watachukia.
"Sub-haana llaah" Mara thelathini na tatu.
"Alhamdulillaah" Mara thelathini na tatu.
"Allaahu Akbaru" Mara thelathini na tatu.
kisha atasema kukamilisha mia moja:
"Laailaha illa llahu wah'dahu laa sharika lahu ,lahulmulku walahulhamdu wahuwa alaa kulli shain qadiir"
Na atasoma suratul Ikhlaswi (Qul huwallaahu) na sura mbili za kinga (Falaq na Nasi) mara tatu baada ya swala ya alfajiri na magharibi, na mara moja baada ya swala zingine.
Na atasoma ayatul kursiy mara moja

Swali: 27- Ni zipi sunna zilizo na mpangilio (Sunani rawatibu)?

Jawabu: Rakaa mbili kabla ya alfajiri.
Rakaa nne kabla ya Adhuhuri.
Rakaa mbili baada ya adhuhuri.
Rakaa mbili baada ya magharibi.
Rakaa mbili baada ya Ishaa.
Ubora wake:
Kasema Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeswali mchana na usiku rakaa kumi na mbili za hiyari, basi Mwenyezi Mungu atamjengea nyumba peponi" Kaipokea Muslim na Ahmad na wengineo.

Swali: 28- Ni ipi siku bora katika siku za wiki?

Jawabu: Ni siku ya ijumaa, Amesema Mtume Sala na amani ziwe juu yake: "Hakika katika siku zenu bora ni siku ya ijumaa, ndani yake kaumbwa Adam, na ndani yake alifariki, na ndani yake litapulizwa baragumu na ndani yake utatokea ukelele, basi zidisheni ndani yake kunitakia rehema juu yangu kwani dua zenu za rehema huletwa kwangu". Akasema: Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni vipi dua zetu zinaletwa kwako na hali tayari uko katika udongo? Akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka ameiharamishia ardhi mili ya Manabii". Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy na wengineo.

Swali: 29- Ni ipi hukumu ya swala ya ijumaa?

Jawabu: Ni faradhi ya lazima kwa kila muislamu mwanaume aliyebalehe mwenye akili na mkazi.
Amesema Allah Mtukufu:
"Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Pindi mwadhini atakapoita kwa ajili ya Swala Siku ya Ijumaa, nendeni upesi msikilize hutuba na mtekeleze Swala, na muache uuzaji na pia ununuaji na kila kinachowashughulisha nyinyi na hiyo Swala. Hilo mliloamrishwa ni bora kwenu nyinyi kutokana na yaliyo humo ya kusamehewa dhambi zenu na kupatiwa malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi iwapo nyinyi mnayajua manufaa ya nafsi zenu, fanyeni hilo". Kwenye aya hii kuna dalili kwamba kwenda kuhudhuria Swala ya Ijumaa na kusikiliza hutuba ni lazima. [Suratul Munafiquun: 9]

Swali: 30- Ni ngapi idadi ya rakaa za swala ya ijumaa?

Jawabu: Idadi ya rakaa za swala ya ijumaa ni mbili, imamu atasoma kwa sauti ndani ya rakaa hizo, kiasi ambacho zitatanguliwa na hotuba mbili zenye kueleweka.

Swali: 31- Je inafaa kutokwenda katika swala ya ijumaa?

Jawabu: Haitakiwi kuacha kwenda katika swala ya ijumaa isipokuwa kwa udhuru wa kisheria, na imekuja kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, kauli yake: "Atakayeacha ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake" Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy na wengineo.

Swali: 32- Taja suna za siku ya ijumaa?

Jawabu:
1- Kuoga.
2- Kutumia manukato.
3- Kuvaa nguo nzuri.
4- Kuwahi mapema msikitini.
5- Kukithirisha kumswalia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.
6- Kusoma suratul kahf.
7- Kwenda msikitini kwa kutembea kwa miguu.
8- Kuitafuta saa ya kujibiwa maombi.

Swali: 33- Taja ubora wa swala ya pamoja.

Jawabu: Kutoka kwa Abdallah bin Omari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Swala ya pamoja ni bora kuliko swala ya mtu mmoja kwa daraja ishirini na saba". Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 34: Nini maana ya kunyenyekea ndani ya swala?

Jawabu: Ni moyo kuhudhuria na viungo kutulia ndani yake.
Amesema Allah Mtukufu:
"Kwa hakika wamefaulu wenye kumuamini Mwenyezi Mungu". "Wale ambao miongoni mwa sifa zao ni kwamba wao ni wanyenyekevu kwenye Swala zao, nyoyo zinajishughulisha na hiyo Swala tu na viungo vyao vimetulia ." [Suratul Mu'uminun: 1,2]

Swali: 35- Elezea maana ya zaka?

Jawabu: Ni haki ya wajibu katika mali maalumu katika wakati maalumu.
- Nayo ni nguzo katika nguzo za uislamu, na ni sadaka ya wajibu inachukuliwa kutoka kwa mwenye uwezo na kupewa fakiri.
Amesema Allah Mtukufu:
(Na toeni zaka) [Suratul Baqara: 43].

Swali: 36- Ni ipi sadaka ya hiyari?

Jawabu: Ni ile isiyokuwa zaka, mfano: kutoa sadaka ya kitu chochote katika njia za kheri katika wakati wowote.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu". [Suratul Baqara: 195].

Swali: 37- Elezea ni nini maana ya swaumu.

Jawabu: Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kujizuia kutokana na vyenye kufunguza kwanzia kuchomoza alfajiri mpaka kuzama jua, pamoja na nia, nayo ina aina mbili:
Swaumu ya wajibu: Mfano: kufunga mwezi wa ramadhani, nayo ni nguzo katika nguzo za uislamu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga saumu kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu." [Suratul Baqara: 183].
Na funga isiyokuwa ya wajibu:
Mfano kufunga siku ya juma tatu na alhamisi kila wiki, na kufunga siku tatu katika kila mwezi, na bora zaidi ni masiku meupe (Tarehe: 13,14,15) katika kalenda ya mwezi (Hijiria).

Swali: 38- Eleza ubora wa kufunga mwezi wa ramadhani.

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Atakayefunga ramadhani kwa imani na kwa kutaraji malipo, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia." Hadithi hii wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 39- Eleza ubora wa swaumu ya hiyari nje ya ramadhani.

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Saidi Al khudriy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Amesema: amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hakuna mja yeyote atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atauweka mbali kwa siku hiyo moja uso wake na moto misimu sabini". Hadithi hii wamekubaliana Bukhari na Muslim.
Maana ya "Misimu sabini" Yaani:
Miaka sabini.

Swali: 40- Taja baadhi ya yanayoharibu swaumu.

Jawabu: Kula na kunywa kwa makusudi.
2- Kujitapisha kwa makusudi.
3- Kuritadi kutoka katika uislamu.

Swali: 41- Ni zipi suna za swaumu?

Jawabu: 1- Kuwahi kufungua.
2- Daku, pamoja na kuichelewesha kwake.
3- Kuongeza juhudi katika amali za kheri miongoni mwa ibada.
4- Kauli ya mfungaji anapotukanwa: Hakika mimi nimefunga.
5- Kuomba dua wakati wa kufuturu.
6- Kufungua kwa tende mbichi au kavu, ikiwa hatopata; basi hata kwa maji.

Swali: 42- Elezea Hijja?

Jawabu: Hija: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kukusudia kwenda katika nyumba yake tukufu kwa ajili ya matendo maalumu na katika wakati maalumu.
Amesema Allah Mtukufu:
{Na Mwenyezi Mungu amewawajibishia watu wafanye Hijja katika nyumba hiyo, yule awezaye kufunga safari kwenda huko, na atakayekanusha (Na asiende na haliyakuwa anauwezo) Basi Mwenyezi Mungu si muhitaji wa kuwahitajia walimwengu} [97]. [Surat Al Imr: 97]

Swali: 43- Ni ngapi idadi ya nguzo za Hija?

Jawabu: 1- Kuhirimia. (kutia nia ya kuanza Hija)
2- Kusimama katika uwanja wa Arafa.
3- Twawafu (Mzunguko katika Alkaaba) wa kumalizia.
4- Kukimbia mchaka mchaka kati ya Swafa na Marwa.

Swali: 3- Ni upi ubora wa Hija?

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akisema: "Mwenye kuhiji na akawa hakusema maneno machafu wala kutenda matendo machafu, anarudi kama alivyo zaliwa na mama yake (akiwa hana dhambi). Ameipokea Bukhari na wengineo.
(Kama siku aliyozaliwa na mama yake) yaani: hana dhambi.

Swali: 45- Elezea Umra?

Jawabu: Umra: Ni kufanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa kukusudia kwenda katika nyumba yake tukufu kwa ajili ya matendo maalumu na katika wakati wowote.

Swali: 46- Ni ngapi idadi ya nguzo za umra?

Jawabu: 1- Kuhirimia. (kutia nia ya kuanza Umra)
2- Kutufu katika nyumba (Alkaaba)
3- Kukimbia mchaka mchaka kati ya Swafa na Marwa.

Jawabu: 47- Ni ipi jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu?

Jawabu: Ni kutoa juhudi na wakati katika kuueneza uislamu na kuutetea na kuwatetea waislamu, au kupigana na adui wa uislamu na waislamu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na piganeni jihadi kwa mali zenu na nafsi zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu ikiwa mnajua" [Suratu Tauba: 41].

Sehemu ya Historia ya Bwana Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake:32

Swali: 1- Ni upi ukoo wa Nabii wetu Muhammadi Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: Naye ni Muhammadi bin Abdillah bin Abil Muttwalib bin Hashim, Na Hashim ni katika makuraishi, na makuraishi ni katika waarabu, na waarabu wanatokana na kizazi cha Ismaili bin Ibrahim kipenzi wa Mwenyezi Mungu kwake na kwa Nabii wetu Amani iwe juu yao.

Swali: 2- Ni lipi jina la mama wa nabii wetu Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: Ni Amina binti Wahabu.

Swali: 3- Alifariki lini baba yake?

Jawabu: Alifarikia baba yake katika mji wa Madina naye (Mtume) akiwa bado ni ujauzito, hajazaliwa Rehema na Amani ziwe juu yake.

Swali: Alizaliwa lini Nabii Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: Katika mwaka wa tembo, siku ya juma tatu mwezi wa Rabi'il Awwal (Mwezi wa tatu katika kalenda ya kiislamu)

Swali: 5- Alizaliwa katika mji gani?

Jawabu: katika mji wa Makka.

Swali: 6- Ni akina nani waliomnyonyesha na kumlea wasiokuwa mama yake?

Jawabu: Aliyeachwa huru na baba yake Mama Ayman.
-Aliyeachwa huru na baba yake mdogo Abuu Lahab, Thuwaiba.
-Halimat Sa'diyya.

Swali: 7- Mama yake alifariki lini?

Jawabu: Alifariki mama yake naye akiwa na umri wa miaka sita, na akamlea babu yake Abdul Muttwalib.

Swali: 8- Ni nani aliyemlea baada ya kifo cha babu yake Abdul Muttwalib?

Jawabu: Alifariki babu yake Abdul Muttwalib naye akiwa ni kijana wa umri wa miaka minane, na akalelewa na baba yake mdogo Abuu Twalib.

Swali: 9- Ni lini alisafiri na baba yake mdogo kwenda Sham?

Jawabu: Alisafiri pamoja na baba yake mdogo kwenda Sham na umri wake ukiwa ni miaka kumi na mbili.

Swali: 10- Ilikuwa lini safari yake ya pili?

Jawabu: Ilikuwa safari yake ya pili ni katika biashara kupitia mali ya bi Khadija Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na aliporudi kutoka safari alimuoa bi khadija, naye akiwa na umri wa miaka ishirini na tano.

Swali: 11- Ni lini walirudishia Makuraishi ujenzi wa Alka'aba?

Jawabu: Walirudishia Makuraishi ujenzi wa Alka'aba, naye akiwa na umri wa miaka thelathini na tano.
Na wakamfanya kuwa hakimu walipotofautiana katika kuliweka jiwe jeusi, akaliweka katika nguo yake, na akaliamrisha kila kabila lishike ncha ya nguo, na yalikuwa makabila manne, walipolinyanyua mpaka mahala pake, akaliweka mwenyewe kwa mkono wake -Rehema na Amani ziwe juu yake.

Swali: 12- Umri wake ulikuwa ni miaka mingapi siku anapewa utume? Na alitumwa kwa watu gani?

Jawabu: Umri wake ulikuwa ni miaka arobaini, na alitumwa kwa watu wote, akiwa mtoa habari njema na muonyaji.

Swali: 13- Ni jambo lipi la kwanza uliloanza nalo wahyi?

Jawabu: Ulianza kwa ndoto za kweli, akawa haoni ndoto isipokuwa ilikuwa ikija mfano wa wingu la asubuhi (ikitokea wazi)

Swali: 14- Ilikuwaje hali yake kabla ya kupewa wahyi? Na ni lini uliteremka wahyi kwake kwa mara ya kwanza?

Jawabu: Alikuwa akifanya ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu katika pango la mlima Hiraa, na alikuwa akichukua chakula cha kumtosha kwa ajili ya hilo.
Na ulimteremkia wahyi, naye akiwa katika pango akifanya ibada.

Swali: 15- Ni kipi cha kwanza kilichoteremka kwake katika Qur'ani?

Jawabu: Ni kauli yake Mtukufu: "Soma, ewe Nabii, Qur’ani uliyoteremshiwa ukianza kwa Jina la Mola wako Aliyepwekeka kwa kuumba." "Aliyemuumba kila binadamu kwa pande la damu nzito nyekundu." "Soma, ewe Nabii, kile ulichoteremshiwa, na Mola wako ni Mwingi wa wema, Mwingi wa ukarimu." "Aliyewafundisha viumbe wake kuandika kwa kalamu." "Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua. Akamtoa kwenye giza la ujinga, Akampeleka kwenye nuru ya elimu." [Suratul A'laq: 1-5].

Swali: 16- Ni nani wa kwanza aliyeuamini ujumbe wake?

Jawabu: katika wanaume: Ni Abuubakari swiddiq, na katika wanawake: Ni Khadija binti Khuwailidi, na katika watoto: ni Ally bin Abii Twalib, na katika waachwa huru: Ni Zaidi bin Haritha, na katika watumwa: Ni Bilali Muhabeshi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na wengineo.

Swali: 17- Ulikuwaje ujumbe wa uislamu?

Jawabu: Ujumbe wa uislamu ulikuwa kwa siri kwa takribani miaka mitatu, kisha akaamrishwa Rehema na amani ziwe juu yake kutangaza ujumbe wazi.

Swali: 18- Ilikuwaje hali ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake na wale waliomuamini baada ya kutangaza wazi ujumbe wake?

Jawabu: Washirikina walipita kiasi katika kumuudhi na kuwaudhi waislamu, mpaka akawaruhusu waumini kuhama kwenda kwa Mfalme Najashi huko Habasha (Ethiopia).
Na wakakubaliana washirikina wote juu ya kumuudhi na kumuua Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, Mwenyezi Mungu akamuhami na akampa ulinzi kupitia baba yake mdogo Abuu Twalib ili amlinde kutokana nao.

Swali: 19- Ni nani aliyefariki katika mwaka wa kumi wa utume wake Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: Alifariki baba yake mdogo Abuu twalib, na mke wake bi Khadija Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Swali: 20- Ni lini ilikuwa safari yake ya usiku ya kupandishwa mbinguni? (israa wal Miiraji)

Jawabu: Alikuwa katika umri wa miaka hamsini, na akafaradhishiwa juu yake swala tano.
Israa (Safari ya usiku): Ilikuwa ni kutoka Msikiti mtukufu wa Makka kwenda Msikiti wa Aqswa (palestina)
(Miiraji) Na kupandishwa: kulikuwa ni kuanzia Msikiti wa Aqswa (Palestina) mpaka katika mbingu ya saba mpaka katika mti wa mkunazi wa mafikio ya mwisho (Sidiratul Muntaha).

Swali: 21- Alikuwa akiwalingania vipi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake watu nje ya Makka?

Jawabu: Alikuwa akiwalingania watu wa Twaifu, na akijitokeza kwao katika misimu mbali mbali na sehemu za mikusanyiko ya watu, mpaka akawaendea watu wa Madina miongoni mwa wale waliomtetea (Maanswari), wakamuamini Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, na wakampa ahadi ya kumnusuru.

Swali: 22- Alikaa muda gani Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akilingania katika mji wa Makka?

Jawabu: Alikaa miaka kumi na tatu.

Swali: 23- Alihamia wapi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: Alihama kutoka Makka kwenda Madina.

Swali: 24- Alikaa Muda gani katika mji wa Madina?

Jawabu: Miaka kumi.

Swali: 25- Ni kitu gani alifaradhishiwa juu yake katika sheria za uislamu?

Jawabu: Alifaradhishiwa juu yake zaka, na swaumu,na Hijja, na Jihadi, na Adhana, na mengineyo miongoni mwa sheria za uislamu.

Swali: 26- Ni vita gani muhimu alipigana mtume?

Jawabu: Ni vita vikuu vya Badri.
Vita vya Uhudi.
Vita vya makundi (Ahzab)
Vita vya ufunguzi wa Makka (Fat-hu Makka)

Swali: 15- Ni kipi cha mwisho kilichoteremka kwake katika Qur'ani?

Jawabu: Ni kauli yake Mtukufu: "Na itahadharini, enyi watu, Siku mtakaporejeshwa kwa Mwenyezi Mungu, nayo ni Siku ya Kiyama, mtakapo orodheshwa kwa Mwenyezi Mungu ili Awahesabu na Amlipe kila mmoja miongoni mwenu kwa alilolitenda la kheri au la shari bila ya kufikiwa na maonevu" [Suratul Baqara: 281].

Swali: 28- Alifariki lini Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake? Na umri wake ulikuwa ni miaka mingapi?

Jawabu: Alifariki katika mwezi wa rabiil Awwal, katika mwaka wa kumi na moja tangu kuhamia Madina, akiwa na umri wa miaka sitini na tatu.

Swali: 29- Taja wake za Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: 1- Khadija binti Khuwailid Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
2- Sauda binti Zam'a Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
3- Aisha binti Abuu Bakari Asswidiiq -Radhi za Allah ziwe juu yake-
4- Hafswa binti Omari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
5- Zainab bint Khuzaima -Radhi za Allah ziwe juu yake.
6- Ummu Salama, Hindu binti Abii Umaiyya Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
7- Ummu Habiba Ramla bint Abii Sufiyaan -Radhi za Allah ziwe juu yake-
8- Juweyriyah bint Al Haarithi - Radhi za Allah ziwe juu yake.
9- Maymuunah bint Al Haarithi - Radhi za Allah ziwe juu yake.
10- Swafiyyah bint Huyeyyi - Radhi za Allah ziwe juu yake.
11- Zainab binti Jahshi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Swali: 30- Ni wapi watoto wake Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: Katika watoto wa kiume ni watatu:
Qassim, na kwa mtoto huyu alikuwa akiitwa.
Na Abdallah.
Na Ibrahim.
Na katika watoto wa kike:

Fatma.
Rukaiyya.
Ummu Kulthum.
Zainab.
Na watoto wake wote hao walizaliwa na Khadija Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, isipokuwa Ibrahim, na wote walifariki kabla yake isipokuwa Fatma alifariki baada yake kwa miezi sita.

Swali: 31- Taja baadhi ya sifa za Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake za kimaumbile?.

Jawabu: Alikuwa Rehema na Amani ziwe juu yake ni wa kati na kati baina ya wanaume, si mfupi wala si mrefu bali alikuwa kati na kati, na alikuwa mweupe aliyechanganyikana na wekundu Rehema na Amani ziwe juu yake, na alikuwa na ndevu nyingi, mwenye macho mapana, mwenye mdomo mzito, na nywele zake zilikuwa nyeusi sana, mwenye mabega mazito, mwenye harufu nzuri, na zinginezo miongoni mwa sifa zake nzuri Rehema na Amani ziwe juu yake.

Swali: 31- Kauacha umma wake katika nini Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: Kauacha umma wake Rehema na Amani ziwe juu yake katika njia nyeupe iliyonyooka, usiku wake ni kama mchana wake, hakuna atakayepotoka katika njia hiyo isipokuwa ataangamia, hakuacha kheri yoyote isipokuwa aliujulisha umma wake katika kheri hiyo, wala shari yoyote isipokuwa aliutahadharisha umma na shari hiyo.

Sehemu ya tafsiri:17

Swali: 1- Soma Suratul Fatiha na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Fatiha na tafsiri yake:
Bismillahir Rahmanir Rahiim (1)" kwa jina la mwenyezi mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu "Alhamdulillaahi Rabbil 'aalamiin" Shukurani zote njema anastahiki mola wa viumbe vyote. "Arrahmaanir rahiim" Mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu "Maaliki yaumid-diin" mfalme wa siku ya malipo. "Iyyaakana'budu wa iyyaakanastaiin" wewe tu ndiye tunayekuabudu na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada . "Ihdinas swiraatwal mustaqiim" Tuongoze njia iliyonyooka. "Swiraatwalladhiina an 'amta a'laihim, ghairil magh dhuubi a'laihim waladh-dhwaalliin" Njia ya wale uliowaneemesha juu yao, na siyo ya wale uliowakasirikia wala ya wale waliopotea. [Suratul- Faatiha 1-7]
Tafsiri:
Imeitwa kuwa ni suratul faatiha (Kifunguzi); kwa sababu ya kukifungua kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa sura hiyo.
🎧 {Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu} Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Yaani: Naanza kisomo cha Qur'ani, kwa kutaka msaada kwake Mtukufu nikitaka baraka kwa kutaja jina lake.
{Allah}. Yaani: Muabudiwa kwa haki, na haitwi mwingine jina hilo zaidi yake Mtukufu.
{Al- rahmaan}: Yaani: Mwenye huruma ya hali ya juu, na yenye kuwaenea viumbe wake wote.
{Al rahiim} Mwenye kurehemu: Yaani: Mwenye kuwahurumia waumini.
🎧 2- {Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu}. Yaani: Aina zote za sifa na ukamilifu ni vya Mwenyezi Mungu peke yake.
🎧 3- {Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu} Yaani: Mwenye huruma pana ambazo zimekienea kila kitu, na mwenye huruma endelevu kwa waumini.
🎧 4- {Mmiliki wa siku ya malipo} Yaani: Ni siku ya kiyama.
🎧 5- {Wewe tu tunakuabudu na wewe tu tunakuomba msaada} Yaani: Tunakuabudu wewe peke yako, na tunakuomba msaada wewe peke yako.
🎧 6- {Tuongoze njia iliyonyooka} Nao ni uongofu wa kuongoka katika uislamu na mafundisho ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.
🎧 7- {Njia ya wale uliowaneemesha juu yao, sio ya wale waliokasirikiwa wala ya wale waliopotea} Yaani: Njia ya waja wema wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii na waliowafuata, na si njia ya wakristo wala Mayahudi.
Na ni sunna mtu aseme baada ya kumaliza kuisoma:
(aamin) Yaani: Tukubalie.

Swali: 2- Soma Suratuz zalzala na uitafsiri.

Jawabu: Suratuz zalzala na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu." "Na ikatoa vilivyomo ndani yake: kama wafu" "Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «leo ardhi ina nini?» "Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo yaliyofanywa juu yake mazuri na mabaya." "kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa." "Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaonyeshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo." "Yeyote mwenye kufanya jema uzito wa mdudu chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera." "Na yeyote mwenye kufanya baya uzito wa punje ndogo atayaona malipo yake Akhera." {Suratuz zalzala: 1-8]
Tafsiri:

🎧 1- "Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu.": Yaani: Itakapotikiswa Ardhi mtikiso mkali utakaotokea siku ya kiyama
🎧 2- "Na ikatoa vilivyomo ndani yake: kama wafu" Na Ardhi ikatoa vilivyo ndani ya tumbo lake miongoni mwa wafu na wengineo.
🎧 3- "Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?» Na mwanadamu atasema katika hali ya kubabaika: Ardhi imekuwaje mbona inatikisika na inagonganagongana?!
🎧 4- "Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya." Katika siku hiyo kubwa Ardhi itaeleza yale yaliyofanywa juu yake miongoni mwa mazuri na ya shari.
🎧 5- "kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa." Kwakuwa Mwenyezi Mungu imefahamisha na akaiamrisha kufanya hivyo.
🎧 "Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaonyeshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo." Katika siku hiyo kubwa ambayo Ardhi itatetemeka ndani yake, watatoka watu kutoka katika kisimamo makundi; Ili wakashuhudie matendo yao waliyoyafanya duniani.
🎧 "Yeyote mwenye kufanya jema uzito wa mdudu chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera." Atakayefanya kwa uzito wa sisimizi jambo dogo katika matendo ya kheri na wema; ataliona mbele yake.
🎧 "Na yeyote mwenye kufanya baya uzito wa punje ndogo atayaona malipo yake Akhera." Na atakayefanya kiasi hicho hicho katika matendo ya shari; basi atakiona mbele yake.

Swali: 2- Soma Aadiyaat na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Aaadiyaati na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda mbio katika njia Yake kumkabili adui, huku wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia." "Wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini." "Wakishambulia wakati wa asubuhi". "Wakirusha vumbi kwa mbio zao." "Wakiwatia kati makundi ya maadui, kwa kuwazunguka kwa vipando vyao, "Hakika binadamu ni mkanushaji sana wa neema za Mola wake." "Na yeye anakubali ukanushaji wake." "Na yeye ana pupa sana ya mali." "Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapo watoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa?" "Na (kwani yeye hajui) kuwa yatatolewa yaliyomo ndani ya vifua: mema au maovu?" "Kwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!" [Suratul Aadiyaat: 1-11]
Tafsiri:
🎧 "Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda mbio katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia." Ameapa Mwenyezi Mungu kwa Farasi ambao wanakwenda mbio mpaka inasikika sauti ya pumzi zao kwa sababu ya kasi kubwa ya kukimbia.
🎧 "Wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini." Na ameapa pia kwa Farasi ambao wanawasha moto kwa kwato zao zinapogusa miamba kwa sababu ya kuikanyaga kwa nguvu.
🎧 "Wakishambulia wakati wa asubuhi" Na amewaapia Farasi ambao wanawashambulia maadui wakati wa asubuhi.
🎧 "Wakarusha vumbi kwa mbio zao." Yaani: Wakatimua vumbi kwa mbio zao.
🎧 "Wakiwatia kati,maadui kuwazunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui" Yaani: Wakalitia kati kwa Farasi zao kundi katika maadui.
🎧 "Hakika binadamu ni mkanushaji sana wa neema za Mola wake." Yaani: Hakika mwanadamu ni mchoyo katika mambo mazuri yale anayoyataka kutoka kwake Mola wake.
🎧 "Na yeye anakubali ukanushaji wake" Na hakika yeye juu ya kuzuia kwake mambo mazuri ni shahidi, hawezi kulipinga hilo kwa sababu liko wazi.
🎧 "Na yeye ana pupa sana ya mali." Yaani: Na hakika yeye ni mkosefu kwa kupenda kwake mali anayoifanyia ubahili.
🎧 "Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa?" Hivi kwani hajui huyu mwanadamu anayedanganyika na uhai wa Dunia kuwa Mwenyezi Mungu atakapoyafufua makaburi katika wafu na akawatoa kutoka katika Ardhi kwa ajili ya hesabu na malipo kuwa jambo halitokuwa kama anavyodhania?!.
🎧 "Na (kwani yeye hajui) kuwa yatatolewa yaliyo ndani ya vifua: mema au maovu?" Na yakawekwa wazi na yakabainishwa yaliyoko ndani ya nyoyo miongoni mwa nia na itikadi na mengineyo.
🎧 "Hakika Mola wao kwao na kwa amali zao, Siku Hiyo, ni Mtambuzi; hakuna chenye kufichikana Kwake" Yaani: Hakika Mola wao katika hilo siku hiyo atakuwa na habari, hakuna chochote kitakachofichikana kwake katika matendo ya waja wake, na atawalipa kwayo.

Swali: 4- Soma Suratu Qari'a na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Qaari'a na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu" "Ni nini kinachogonga" "Ni kipi kinachokujuza ni kipi kinachogonga?" "Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama panzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni." "Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa ni mapepe na ikamalizika." "Basi mwenye kuwa mizani ya mema yake ni nzito," "atakuwa kwenye maisha ya kuridhika Peponi." "Ama mwenye kuwa mizani ya mema yake ni nyepesi na mizani ya maovu yake ni nzito" "Basi makazi yake yatakuwa ni moto wa Hawiya" "Ni kipi kinachokujuza ni upi moto wa Hawiya?" "Ni moto mkali" [Suratul Qaria: 1-11]
Tafsiri:
🎧 "Kiyama kigongacho" Kiyama kinachogonga nyoyo za watu kwa ukubwa wa vitisho vyake.
🎧 "Ni nini kigongacho" Ni muda gani huu ambao utagonga nyoyo za watu kwa ukubwa wa vitisho vyake?!
🎧 "Na nini kitakachokujulisha ni kipi kigongacho?" Ni kipi kilichokufahamisha ewe Mtume ni saa gani hii ambayo inagonga nyoyo za watu kwa ukubwa wa vitisho vyake?! Hiyo ni siku ya kiyama.
🎧 "Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama panzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni." Siku ambayo itagonga nyoyo za watu watakuwa mfano wa panzi waliotawanyika wanaozagaa huku na kule.
🎧 "Na milima itakuwa kama sufi iliyotawanywa" Na itakuwa milima mfano wa sufi iliyochambuliwa kulingana na wepesi wa kupeperuka kwake na kutembea kwake.
🎧 "Ama itakayekuwa mizito mizani yake":
Ama ambaye matendo yake mema yatazidi matendo yake mabaya.
🎧 "Basi huyo atakuwa katika maisha ya kuridhika":
Yaani atakuwa katika maisha ya kuridhika atakayoyapata peponi.
🎧 "Ama itakayekuwa mwepesi mizani yake":
Ama ambaye matendo yake maovu yatazidi matendo yake mema.
🎧 "Basi makazi yake ni moto wa Hawiya" Yaani:
Maskani yake na makazi yake siku ya kiyama ni Jahanamu.
🎧 "Ni nini kitakachokujulisha ni ipi hiyo Hawiya":
Ni kipi kitakachokufahamisha ewe Mtume ni ipi hiyo?!
🎧 "Ni moto mkali": Nao ni moto wenye joto kali.

Swali: 5- Soma Suratut Takaathur na uitafsiri.

Jawabu: Suratut Takaathur na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Kumekushughulisheni kutaka wingi" "Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkawa makaburini na mkazikwa humo." "Siyo namna hii kunatakiwa kuwapumbaze kushindana kwa wingi wa mali. Itawadhihirikia kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu." "Kisha tahadharini mtajua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera." "Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali. Lau mnajua ukweli, mngalirudi nyuma na mngalishughulika na kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu." "Hakika bila shaka mtauona moto wa Jahanam" "Kisha mtauona bila shaka!" "Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo." [Suratut Takaathur: 1-8]
Tafsiri:
🎧 "kumekushughulisheni kutaka wingi": Kumekushughulisheni enyi watu kujifaharisha kwa mali na watoto mkaacha kumtii Mwenyezi Mungu.
🎧 "Mkaendelea kujishughulisha kwenu mpaka mkaingia makaburini" Yaani:
Mpaka mkafa mkaingia makaburini mwenu.
🎧 "Si hivyo, mtakuja jua" Hamkutakiwa kuwashughulishe huko kujifaharisha kwa hayo mkaacha kumtii Mwenyezi Mungu, mtakuja kujua mwisho wa huko kujishughulisha.
🎧 "Kisha, si hivyo, mtakuja jua": Mtakuja jua mwisho wake.
🎧 "Si hivyo, lau mngelijua kikweli kweli": Yaani: Kiukweli laiti mngelijua kwa hakika kuwa nyinyi mtafufuliwa mbele ya Mwenyezi Mungu, nakuwa yeye atakulipeni juu ya matendo yenu, kwa kitendo chenu cha kujishughulisha na kujifaharisha kwa mali na watoto.
🎧 "Hakika bila shaka mtauona moto wa Jahim" Namuapa Mwenyezi Mungu mtaushuhudia moto siku ya kiyama.
🎧 "Kisha hakika mtauona bila shaka" Kisha mtaushuhudia kuushuhudia kwa uhakika kusikokuwa na shaka ndani yake.
🎧 "Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo." Kisha bila shaka atakuulizeni Mwenyezi Mungu katika siku hiyo juu ya yale aliyokuneemesheni miongoni mwa afya na utajiri na mengineyo.

Swali: 6- Soma Suratul Asri na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Asri na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Na apa kwa wakati wa laasiri" "Hakika wanadamu wako kwenye maangamivu na upungufu". "Isipokuwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakafanya matendo mema, wakausiana wao kwa wao kushikamana na haki, kufanya matendo ya kumtii Mwenyezi Mungu na kusubiri juu yake" [1]. [Suratul Asri: 1-3]
Tafsiri:
🎧 "Na apa kwa wakati wa laasiri": Ameapa Mtukufu kwa nyakati.
🎧 "kwamba wanadamu wako kwenye maangamivu na upungufu". Yaani: Kila mwanadamu yuko katika mapungufu na maangamivu.
🎧 "Isipokuwa wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakafanya amali njema, wakausiana wao kwa wao kushikamana na haki, kufanya matendo ya kumtii Mwenyezi Mungu na kusubiri juu yake" Isipokuwa yule atakayeamini na akafanya matendo mema, na pamoja na hilo walingania katika haki na wakasubiri juu ya hilo, hawa ndio waliookoka na hasara.

Swali: 7- Soma Suratul Humaza na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Humaza na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatukana." "Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuyahesabu." "Akidhani kuwa mali yake ambayo ameikusanya itampa dhamana ya kuishi milele duniani na kukwepa kuhesabiwa." "Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa." "Ni kipi kinachokujuza ni kipi kinachovunja vunja?" "Huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa." "Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini ukafikia kwenye nyoyo." "Moto huo umefungiwa juu yao wakiwa wametiwa minyororo" "Na pingu ndefu ili wasitoke." [Suratul Humaza: 1-9]
Tafsiri:
🎧 "Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatukana." Tatizo kubwa na adhabu kali kwa mtu anayewasengenya watu kwa wingi, na kuwasema vibaya.
🎧 "Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuyahesabu.": Ambaye pupa yake ni kukusanya mali na kuzihesabu, hana malengo mengine zaidi ya hayo.
🎧 "Akidhani kuwa mali yake ambayo ameikusanya itampa dhamana ya kuishi milele duniani na kukwepa kuhesabiwa." Anadhani kuwa mali yake aliyoikusanya itamuokoa na mauti, kuwa atabakia milele katika maisha ya dunia.
🎧 "Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa." Uhakika si kama anavyofikiria huyu mjinga, Hakika atatupwa katika moto wa Jahanam ambao unagonga na kukivunja kila kinachorushwa ndani yake kwa ukubwa wa ugumu wake.
🎧 "Ni kipi kinachokujuza ni kipi kinachovunja vunja?" Na ni kipi kilichokufahamisha ewe Mtume ni upi moto huu ambao unavunjavunja kila kinachotupwa ndani yake?!
🎧 "Huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa." Huo ni moto wa Mwenyezi Mungu uliochochewa.
🎧 "Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini ukafikia kwenye nyoyo." Ambao unapenyeza katika mili ya watu na kufika mpaka katika nyoyo zao.
🎧 "Moto huo umefungiwa juu yao wakiwa wametiwa minyororo" Hakika moto huo umefungwa juu ya wale wenye kuadhibiwa ndani yake.
🎧 "na pingu ndefu ili wasitoke." Kwa nguzo imara ndefu ili wasiweze kutoka ndani yake.

Swali: 8- Soma suratul Fil na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Fil na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu?" "Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu?" "Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana, ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu." Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa." [Suratul Fil: 1-5.]
Tafsiri:
🎧 "Je hujui, ewe Mtume, namna Alivyowafanya Mola wako watu wa ndovu: Abraha Mhebeshi na jeshi lake ambalo alikuja nalo ili kuivunja Alkaba tukufu?" Hivi hujui ewe Mtume ni jinsi gani alimfanya Mola wako Abraha na watu wa ndovu walipotaka kuibomoa Alkaaba?!
🎧 "Kwani Hakuijaalia mipango yao mibaya waliyoifanya ni yenye kuvunjika na kupita patupu?" Aliifanya Mwenyezi Mungu mipango yao mibaya ya kuibomoa kuwa ni hasara, hawakufanikisha walilotamani la kuwaondoa watu katika Alkaaba, na wala hawakufanikisha chochote.
🎧 "Na Aliwapelekea makundi yaliyofuatana," Na akawatumia ndege, waliowajia makundi kwa makundi.
🎧 ya ndege waliokuwa wakiwatupia wao vijiwe vya udongo mkavu mgumu." Waliwapiga kwa mawe ya udongo mgumu.
🎧 Akawapondaponda, wakawa ni kama majani makavu yaliyoliwa na wanyama na halafu kutupwa." Mwenyezi Mungu akawafanya kama majani ya mimea yaliyotafunwa na mnyama na akayakanyaga.

Swali: 9- Soma Suratu Quraishi na uitafsiri.

Jawabu: Suratu Quraishi na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
(Kwa ajili ya kuzoea Makuraishi) (1) (Kuzoea kwao misafara ya kusi na kaskazi) (2) "Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Alkaaba, Ambaye kwa ajili Yake wametukuzwa, na wampwekeshe na kumtakasia ibada." "Ambaye Amewapa wao chakula wakati wa njaa kali na akawapa amani na utulivu kutokana na hofu kubwa na mbabaiko." [Suratu Quraishi: 1-4]
Tafsiri:
🎧 (Kwa ajili ya kuzoea Makuraishi) (1) Makusudio ya hilo na kile walichokuwa wamekizoea miongoni mwa safari za masika na kiangazi.
🎧 (Kuzoea kwao misafara ya kusi na kaskazi) (2) Safari ya masika walikuwa wakienda Yemen, na safari ya kiangazi walikuwa wakienda Sham (Siria, iraq, Jordan, Palestina) wakiwa na amani.
🎧 "Basi, wamshukuru na kumuabudu Bwana wa Nyumba hii ya Alkaaba, Ambaye kwa ajili Yake wametukuzwa, na wampwekeshe na kumtakasia ibada." Basi na wamuabudu Mwenyezi Mungu Mola wa nyumba hii peke yake, aliyewafanyia wepesi safari hizi, na wala wasimshirikisha na yeyote.
🎧 "Ambaye Amewapa wao chakula wakati wa njaa kali na akawapa amani na utulivu kutokana na hofu kubwa na mbabaiko." Aliyewalisha wakati wa njaa, na akawapa amani na kuwaondolea hofu, kwa kile alicho kiweka katika nyoyo za waarabu kwa sababu ya utukufu wa msikiti mtukufu, basi walikuwa wakiwatukuza wakazi wa maeneo ya msikiti huo mtukufu.

Swali: 10- Soma Suratul Maauun na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Maaun na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa?" "Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake." "Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha?." "Adhabu kali itawathibitikia wenye kusali" (4) "ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake." "Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria." "Na wanazuia misaada" [Suratul Maauun: 1-7]
Tafsiri:
🎧 "Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa?" Je umemfahamu anayekanusha kuwepo malipo na siku ya kiyama?
🎧 "Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake." Huyo ni yule anayemsukuma yatima kwa ukali anapokuwa na haja.
🎧 "Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha?." Na wala haihimizi nafsi yake, wala hamuhimizi mwingine juu ya kulisha masikini.
🎧 "Adhabu kali itawathibitikia wenye kusali" (4) Maangamivu na adhabu kwa wenye kuswali.
🎧 "ambao wameghafilika na Swala zao:
hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake." Ambao huzipuuza swala zao, hawazijali mpaka wakati wake unapomalizika.
🎧 "Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria." Ambao hujionyesha kwa swala zao na matendo yao, hawatakasi matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
🎧 "Na wanazuia misaada":
Na wanazuia kuwasaidia wengine kwa vitu ambavyo haviwadhuru endapo watawasaidia.

Swali: 11- Soma Suratul Kauthar na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Kauthar na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Hakika sisi tumekupa, ewe Nabii, kheri nyingi za dunia na Akhera." "Basi, swali na uchinje kwa ajili ya mola wako pekee". "Hakika mwenye kukuchukia wewe na kuyachukia uliyokuja nayo ya uongofu na nuru ndiye aliyekatiwa kila kheri." [Suratul Kauthar: 1-3]
Tafsiri:
🎧 "Hakika sisi tumekupa, ewe Nabii, kheri nyingi za dunia na Akhera, miongoni mwazo ni mto wa Kauthar ulioko Peponi ambao pambizo zake ni mahema ya lulu na mchanga wake ni miski." Hakika sisi tumekupa ewe Mtume kheri nyingi, na miongoni mwake ni mto wa kauthar ulioko peponi.
🎧 "Basi,swali na uchinje wako kwa ajili ya mola wako
, Peke Yake, pamoja na kutaja jina Lake" Tekeleza shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa neema hii, usali kwa ajili yake peke yeke na uchinje kwa ajili yake, kinyume na vile wanavyofanya washirikina kwa kujikurubisha katika masanamu yao kwa kuyachinjia.
🎧 "Hakika mwenye kukuchukia wewe na kuyachukia uliyokuja nayo ya uongofu na nuru ndiye itakayekatika athari yake na yeye mwenyewe kukatiwa kila kheri." Hakika mwenye kukuchukia ndiye aliyekatikiwa na kila kheri, aliyesahaulika ambaye akitajwa anatajwa kwa ubaya.

Swali: 12- Soma Suratul Kaafirun na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Kaafiruun na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliokufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu!" «Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa uongo." «Wala nyinyi si wenye kumuabudu ninayemuabudu.» «Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa uongo." «Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» «Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.» [Suratul Kaafiruun: 1-6]
Tafsiri:
🎧 «Sema, Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu!" Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliomkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake
🎧 «Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa uongo." Siabudu kwa wakati huu wala wakati ujao mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu.
🎧 «Wala nyinyi si wenye kumuabudu ninayemuabudu.»
Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu mimi, naye ni Allah peke yake.
🎧 «Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa uongo." Wala mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu.
🎧 «Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.»
Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu mimi, naye ni Allah peke yake.
🎧 «Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.» Nyinyi mna dini yenu mliyoizusha nyinyi wenyewe, na mimi nina dini yangu aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu juu yangu.

Swali: 13- Soma Suratun Nasri na uitafsiri.

Jawabu: Suratun Nasri na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Utakapotimia kwako ewe Mtume, ushindi juu ya makafiri wa Kikureshi na ukaufungua mji wa Makkah." "Na ukaona watu wengi wanaingia kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi." "Yatakapotokea hayo, jitayarishe kukutana na Mola Wako kwa kumtakasa, kumhimidi na kumuomba msamaha kwa wingi. Kwani Yeye ni Mwingi wa kuwakubalia toba wenye kumsabihi na kumuomba msamaha, kwa kuwasamehe na kuwarehemu." [Suratun Nasri: 1-3]
Tafsiri:
🎧 "Utakapotimia kwako ewe Mtume, ushindi juu ya makafiri wa Kikureshi na ukaufungua mji wa Makkah." Utakapokuja msaada wa Mwenyezi Mungu kwa dini yako ewe Mtume- na utukufu wake, na ukatokea ufunguzi wa Mji wa Makka.
🎧 "Na ukaona watu wengi wanaingia kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi." Na ukawaona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi.
🎧 "Yatakapotokea hayo, jitayarishe kukutana na Mola Wako kwa kumtakasa, kumhimidi na kumuomba msamaha kwa wingi. Kwani Yeye ni Mwingi wa kuwakubalia toba wenye kumsabihi na kumuomba msamaha, kwa kuwasamehe na kuwarehemu." Basi tambua kuwa hiyo ni alama ya kukaribia kumalizika kwa muda wa kutumwa kwako, basi mtakase mola wako kwa kumshukuru juu ya neema ya ushindi, na kutake kwake msamaha, hakika yeye ni mwingi wa kukubali toba za waja wake, na kuwasamehe.

Swali: 14- Soma Suratul Masad na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Masad na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Imepata hasara mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia" "Haikumfaa mali yake wala alichokichuma" "Ataingia kwenye Moto wenye muwako mkali," "Yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi." "Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara iliyosokotwa; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini." [Suratul Masad: 1-5.]
Tafsiri:
🎧 "Imepata hasara mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia" Imepata asara mikono ya baba yake mdogo na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, Abuu Lahab bin Abdil Muttwalib kwa hasara aliyoipata ammi yake, kwani alikuwa akimuudhi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, na zimebatilika juhudi zake.
🎧 "Haikumfaa mali yake wala alichokichuma":
Ni kitu gani zimemsaidia mali zake na watoto wake? Hazijamkinga na adhabu, wala hazijamletea rehema.
🎧 "Ataingia kwenye Moto wenye muwako mkali," Atauingia siku ya kiyama moto wenye muwako, akichomwa kwa joto lake.
🎧 "Yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi." Na atauingia mkewe mama Jamil aliyekuwa akimuudhi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, kwa kumtupia miba katika njia yake.
🎧 "Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara iliyosokotwa; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini.": Shingoni mwake kuna kamba nzito iliyokazwa atakuwa akikokotwa nayo kwenda motoni.

Swali: 15- Soma Suratul Ikhlaswi na uitafsiri.

Jawabu: Suratul Ikhlaswi na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Sema, ewe Mtume, «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo." "Mwenyezi Mungu ndiye mkusudiwa" (2) «Hakuzaa wala hakuzaliwa" «Wala hakuna yeyote katika viumbe vyake mwenye kufanana wala kushabihiyananaye katika majina yake, sifa zake wala vitendo vyake.» [Suratul Ikhlaswi: 1-4]
Tafsiri:
🎧 "Sema, ewe Mtume, «Yeye ndiye Mwenyezi Mungu aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo.": Sema ewe Mtume- Yeye ndiye Mwenyezi Mungu hakuna mungu zaidi yake.
🎧 "Mwenyezi Mungu tu ndiye mkusudiwa":
Yaani: Hupelekwa kwake shida zote za viumbe.
🎧 "Hakuzaa na wala hakuzaliwa":
Hana mtoto Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka na wala hana mzazi.
🎧 "Na wala hakuna yeyote anayefanananaye hata mmoja":
Na wala hajawahi kuwa na mfano wake katika viumbe wake.

Swali: 16- Soma Suratul Falaq na uitafsiri.

Jawabu: Suratut Falaq na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
Sema «Najilinda kwa mola wa mapambazuko". «Kutokana na shari la viumbe na udhia wao" «Na shari ya usiku wenye giza jingi uingiapo na ujikitapo na shari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake." «Na shari ya wachawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga." «Na shari ya hasidi mwenye kuchukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Alizowaneemesha ziwaondokee.» [Suratul Falaq: 1-5].
Tafsiri:

🎧 Sema «Najilinda kwa mola wa mapambazuko". Sema ewe Mtume- Najikabidhi kwa Mola muumba wa asubuhi, na ninajiweka karibu kwake.
🎧 "Kutokana na shari ya vile alivyoumba":
Kutokana na shari ya vile vyenye kuudhi katika viumbe vyake.
🎧 «Na shari ya usiku wenye giza jingi uingiapo na ujikitapo na shari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake.": Najikabidhi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari ambazo zinajitokeza usiku miongoni mwa wanyama na wezi.
🎧 «Na shari ya wachawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga.": Na ninajikabidhi kwake kutokana na shari za wanga ambao hupuliza katika mafundo wanaporoga.
🎧 «Na shari ya hasidi mwenye kuchukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Alizowaneemesha ziwaondokee.»
Na kutokana na shari za hasidi mwenye kuwachukia watu anapowahusudu juu ya yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika neema, akitaka ziwaondokee, na kuwatia maudhi.

Swali: 17- Soma Suratun Nas na uitafsiri.

Jawabu: Suratun Nas na tafsiri yake:
Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake.
"Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu" "Mfalme wa watu" (2) "Mola wa watu" «Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu." «Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu." «Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.» [Suratun Nas: 1-6]
Tafsiri:
🎧 Sema «Najilinda kwa mola wa watu". Sema ewe Mtume- Najikabidhi kwa Mola muumba wa asubuhi, na ninajiweka karibu kwake.
🎧 "Mfalme wa watu":
Anafanya maamuzi yoyote kwao kwa ayatakayo, hawana mmiliki mwingine zaidi yake.
🎧 "Mola wa watu":
Muabudiwa wao wa haki, hawana muabudiwa wa kweli mwingine zaidi zake.
🎧 «Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu." Kutokana na shari za shetani ambaye anatia wasi wasi wake kwa watu.
🎧 «Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu." Anapenyeza kwa wasi wasi wake katika nyoyo za watu.
🎧 «Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.»
Yaani: Mwenye kutia wasi wasi anakuwa katika binadamu na anakuwa katika majini.

Sehemu ya Hadithi:14

Swali 1-: kamilisha hadithi: "Hakika bila shaka amali zote huzingatiwa nia" na eleza baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa kiongozi wa waumini Abuu Hafsi Omari bin Khattwab Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu Rehema na Amani ziwe juu yake akisema: "Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilolinuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi (malipo yake yatakuwa) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya dunia ataipata, au kwa ajili ya mwanamke ili amuoe, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa lile alilolihamia". Ameipokea Bukhari na Muslim.
Faida zinazo patikana katika hadithi
1- Kila matendo lazima yawe na nia, kama swala, na swaumu, na Hijja, na matendo mengine.
2- Ni lazima kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Hadithi ya pili:

Kamilisha hadithi: "Atakayezua katika jambo letu hili" na eleza baadhi ya faida zake?

Jawabu: Kutoka kwa mama wa waumini mama Abdillah Aisha Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake "Yeyote atakayezua katika jambo letu hili (Dini yetu hii) jambo ambalo si katika dini hii basi atarejeshewa jambo hilo alilolizua" Ameipokea Bukhari na Muslim.
Faida zinazo patikana katika hadithi
1- Katazo la kuzua katika dini.
2- Na yakwamba matendo yote yenye kuzushwa hurejeshwa na hayakubaliki.
Hadithi ya tatu:

Swali: 3- kamilisha hadithi: "Tukiwa tumekaa kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake" Na eleza baadhi ya faida zake?.

Jawabu: Kutoka kwa Omar Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: "Tukiwa sisi tumekaa kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- siku moja, ghafla akatokeza mwanaume mmoja, mwenye nguo nyeupe sana, mwenye nywele nyeusi sana, hazionekani kwake athari za safari, na wala hakuna anayemfahamu yeyote katika sisi, mpaka akakaa kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akashikanisha magoti yake na magoti mtume Rehema na Amani ziwe juu yake (mfano wa kikao cha tahiyatu) na akaweka mikono yake juu ya mapaja yake, Na akasema: Ewe Muhammadi, nieleze kuhusu Uislamu? Akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: Uislamu ni kushuhudia kuwa hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa ni Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na udumishe swala na utoe zaka, na ufunge Ramadhani, na uhiji nyumba tukufu ukipata uwezo wa kuifikia, Yule bwana akasema: "Swadakta"-Yaani: Umesema kweli, Tukamshangaa! Anamuuliza na anamsadikisha! Akasema: Nieleze kuhusu Imani? Akasema: Ni kumuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho, na uamini makadirio kheri yake na shari yake, Akasema: "Swadakta"-Yaani: Umesema kweli, Basi hebu nieleze kuhusu Ihsani (wema)? Akasema: Ni umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba wewe unamuona, na kama wewe humuoni basi yeye anakuona: Akasema: Hebu nieleze kuhusu kiyama: Akasema: hakuwa muulizwaji kuhusu hilo ni mjuzi kuliko muulizaji, Akasema: Hebu nieleze kuhusu dalili zake? Akasema: ni mjakazi kuzaa bwana wake, na ukawaona watembea peku,uchi na masikini wachunga mifugo wakishindana kujenga majengo marefu, kisha yule bwana akaondoka, akakaa muda kidogo kisha akasema: Ewe Omari unamjua ni nani huyo muulizaji? Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, Akasema: Basi bila shaka huyo ni Jibril alikuja ili akufundisheni dini yenu". Imepokelewa na Imamu Muslim
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Kumetajwa ndani yake nguzo tano za uislamu; nazo ni:
1- Ni kushuhudia kuwa hapana mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake na muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
2- Na kudumisha swala.
3- Na kutoa zaka.
4- Kufunga ramadhani.
5- Na kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu.
2- kumetajwa nguzo za imani, nazo ni sita:
Kumuamini Mwenyezi Mungu.
Na Malaika wake.
Na vitabu vyake.
Na Mitume wake.
Na siku ya mwisho.
6- Na makadirio kheri yake na shari yake.
3- Kumetajwa nguzo za ihsan, nayo ni nguzo moja, nayo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kama unamuona, na ikiwa wewe humuoni basi yeye anakuona.
4- Wakati wa kusimama kiyama, hakuna aujuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Hadithi ya nne:

Swali 4-: kamilisha hadithi: "Muumini mwenye imani kamili kuliko wote" na eleza baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: amesema: Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Muumini aliyekamilika kiimani ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine". Kaipokea Tirmidhiy na akasema: Hadithi ni nzuri na ni sahihi".
Faida zinazo patikana katika hadithi
1- Himizo la kuwa na tabia njema.
2- Na yakwamba ukamilifu wa tabia ni katika ukamilifu wa imani.
3- Na yakwamba imani inaongezeka na kupungua.
Hadithi ya tano:

Swali: 5- Kamilisha hadithi: "Atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu" Na ueleze baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Abdallah bin Omari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, ya kwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake amesema: "Mwenye kumuapia asiyekuwa Allah atakuwa amekufuru au kamshirikisha Allah." Kaipokea Imamu Tirmidhiy
Faida zinazo patikana katika hadithi
-Hafai kuapa isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni katika shirki ndogo.
Hadithi ya sita:

Swali: 6- Kamilisha hadithi: "Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka nipendeke kwake" Na eleza baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Anasi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka niwe napendeka zaidi kwake kuliko mtoto wake, mzazi wake, na watu wote." Ameipokea Bukhari na Muslim.
Faida zinazo patikana katika hadithi:

- Kumpenda Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake ni wajibu kuliko mapenzi ya watu wote.
- Na yakwamba hilo ni katika ukamilifu wa imani.
Hadithi ya saba:

Swali: 7- Kamilisha hadithi: "Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake" Na eleza baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Anasi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake" Ameipokea Bukhari na Muslim.
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Ni juu ya muumini kuwapendelea waumini kheri kama anavyoipendelea nafsi yake.
- Na hilo ni katika ukamilifu wa imani.
Hadithi ya nane:

Swali 8-: kamilisha hadithi: "Namuapia yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake" na eleza baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudry Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake amesema: "Namuapia yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake! Hakika hiyo inalingana na theluthi ya Qur'ani" Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Ubora wa suratul Ikhlaswi.
2- Nakwamba sura hiyo inalingana na theluthi ya Qur'ani.
Hadithi ya tisa:

Swali: 9- Kamilisha hadithi: "Hakuna ujanja wala kuwa na nguvu isipokuwa zinatoka kwa Mwenyezi Mungu" Na eleza baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Mussa Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Neno 'Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah' Hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa zinatoka kwa Mwenyezi Mungu, ni hazina miongoni mwa hazina za pepo" Ameipokea Bukhari na Muslim.
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Ubora wa neno hili, nakwamba neno hili ni hazina miongoni mwa hazina za pepo.
2- Linamuweka mbali mja na ujanja wake na nguvu zake, na kutegemea kwake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake.
Hadithi ya kumi:

Swali: 10- Kamilisha hadithi: "Tambueni kuwa hakika katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama" na eleza baadhi ya faida zake?

Jawabu: Kutoka kwa Nuaim bin Bashiri Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nilimsikia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akisema: "Tambueni kuwa hakika katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama kitakapotengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika mwili mzima una haribika, tambueni, kipande hicho ni moyo" Ameipokea Bukhari na Muslim.
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Kutengemaa kwa moyo ndani yake kunapelekea kutengemaa kwa mtu nje na ndani.
2- Kutilia umuhimu kurekebisha moyo, kwa sababu moyo ndiyo unaomfanya mtu atengemae.
Hadithi ya kumi na moja:

Swali: 11- kamilisha hadithi: "Yatakayekuwa maneno yake ya mwisho duniani ni: Laa ilaaha illa llaah- Hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu" Na eleza baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Muadh bin Jabal Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Yatakayekuwa maneno yake ya mwisho duniani ni: Laa ilaaha illa llaah- Hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu ataingia Peponi". Imepokelewa na Abuu Daud
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Ubora wa neno, Laa ilaaha illa llaahu, nakwamba mja ataingia peponi kwa neno hilo.
2- Na ubora wa mtu ambaye yatakuwa maneno yake ya mwisho kutoka duniani ni Laa ilaaha illa llaahu.
Hadithi ya kumi na mbili:

Swali: 12- Kamilisha hadithi: "Muumini si msemaji wa watu vibaya, wala mtoa laana" Na baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Abdilah bin Masoud Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Muumini si msemaji watu vibaya, wala mtoaji wa laana, wala muovu, wala mwenye kauli chafu" Kaipokea Imamu Tirmidhiy
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Katazo la maneno yote ya batili na machafu.
-Na yakwamba hiyo ndiyo sifa ya muumini katika ulimi wake.
Hadithi ya kumi na tatu:

Swali: 13- Kamilisha hadithi: "Katika uzuri wa uislamu wa mtu" Na ueleze baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: amesema: Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu" Kaipokea Tirmidhiy.
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Mtu kuyacha yasiyomuhusu katika mambo ya dini ya mtu mwingine au dunia yake.
2- Kuacha yasiyomuhusu ni katika ukamilifu wa uislamu wake.
Hadithi ya kumi na nne:

Swali: 14- Kamilisha hadithi: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu" Na eleza baadhi ya faida zake.

Jawabu: Kutoka kwa Abdillah bin Masoud: Yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, amesema: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema moja hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi: Alif Laam Miim ni herufi moja, Lakini, alifu ni herufi, na Laam ni herufi, na Miim ni herufi" Kaipokea Imamu Tirmidhiy
Faida zinazo patikana katika hadithi:

1- Ubora wa kusoma Qur'ani.
2- Na yakwamba kwa kila herufi unayoisoma unapata mema mengi kwa herufi hiyo.

Sehemu ya Adabu za kiislamu:26

Swali: 1- Inakuwaje adabu pamoja na Mwenyezi Mungu Mtukufu?

Jawabu: 1- Kwa kumtukuza yeye aliyetakasika na kutukuka.
2- Kwa kumuabu yeye pekee asiye na mshirika.
3- Kumtii.
4- Kuacha kumuasi.
5- Kumshukuru na kumsifu yeye Mtakasifu juu ya fadhila zake na neema zake ambazo hazihesabiki.
6- Na kusubiri juu ya makadirio yake.

Swali: 2- Inakuwaje adabu pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake?

Jawabu: 1- Kwa kumfuata na kuiga kutoka kwake.
2- Kwa kumtii.
3- Kuacha kumuasi.
4- Kumsadikisha katika yale aliyoyaeleza.
5- Kuacha uzushi kwa kuongeza juu ya muongozo wake.
6- Kumpenda zaidi kuliko nafsi na watu wote.
7- Kumuheshimu na kumtetea na kuyatetea mafundisho yake.

Swali: 3- Inakuwaje adabu pamoja na wazazi wawili?

Jawabu: 1- Kuwatii wazazi wawili katika yale ambayo si maasi.
2- Kuwahudumia wazazi.
3- Kuwasaidia wazazi.
4- Kukidhi mahitaji ya wazazi.
5- Kuwaombea dua wazazi.
6- Kuwa na adabu wakati wa maongezi; Haitakiwi kusema: "Ahh!", nayo ni kauli ndogo zaidi.
7- Kutabasamu katika uso wa wazazi wawili na wala siyo kukunja sura.
8- Sinyanyui sauti yangu juu ya sauti ya wazazi wawili, na nina wasikiliza, na wala siwakatishi kwa mazungumzo, na wala siwaiti kwa majina yao, bali ninasema: "Baba yangu", "Mama yangu".
9- Ninaomba ruhusa kabla ya kuingia ndani kwa baba yangu na mama yangu wakiwa chumbani.
10- Nabusu kichwa na mkono wa wazazi wawili.

Swali: 4- Nitaunga vipi udugu?

Jawabu: 1- Kwa kuwatembelea ndugu wa karibu kama kaka na dada, na baba mdogo au mkubwa na shangazi, na mjomba, na mama mdogo au mkubwa, na ndugu wengine wa karibu.
2- Kuwafanyia wema kwa kauli na vitendo, na kuwasaidia.
3- Na miongoni mwake ni kuwasiliana nao na kuwauliza hali zao.

Swali: 5- Ni vipi nitaishi na ndugu zangu na marafiki zangu?

Jawabu: 1- Kwa kuwapenda na kuambatana na marafiki wazuri.
2- Ninajiepusha na ninaacha kuambatana na waovu.
3- Ninawasalimia ndugu zangu na ninawapa mikono.
4- Ninawatembelea wanapougua na ninawaombea dua ya shifaa.
5- Na ninamuombea rehema anayepiga chafya.
6- Na ninaitika wito wake anaponiita kwa ajili ya kumtembelea.
7- Ninampa nasaha.
8- Ninamnusuru anapodhulumiwa, na ninamzuia na dhulma.
10- Ninampendelea ndugu yangu muislamu yale ninayoipendelea nafsi yangu.
11- Ninamsaidia anapohitaji msaada wangu.
12- Simfanyii maudhi, kwa kauli na vitendo.
13- Ninahifadhi siri yake.
14- Simtukani, na wala simsengenyi, au kumdharau, au kumuhusudu, na wala simpelelezi, au kumfanyia ghushi.

Swali: 6- Ni zipi adabu za ujirani?.

Jawabu: 1- Ninamfanyia wema jirani kwa kauli na vitendo, na ninamsaidia anapohitaji msaada wangu.
2- Ninampongeza anapokuwa katika furaha ya sikukuu au ndoa na mengineyo.
3- Ninamtembelea anapougua, ninampa pole anapopatwa na msiba.
4- Na ninampelekea kile ninachokipika katika chakula kwa kiasi ninachokiweza.
5- Simpatii maudhi kwa kauli au vitendo.
6- Simsumbui kwa sauti ya juu, au kumpeleleza, na ninamvumilia.

Swali: Ni zipi adabu za ugeni na mgeni?

Jawabu: 1- Ninamkubalia anayeniita kwa ajili ya kuwa mgeni kwake.
2- Ninapotaka kumtembelea yeyote ninamtaka idhini na ahadi pia.
3- Ninaomba ruhusa kabla ya kuingia.
4- Sichelewi kumtembelea
5- Na ninainamisha macho kwa watu wa familia yake.
6- Ninamkaribisha mgeni na ninampokea kwa mapokezi mazuri, kwa uso mkunjufu na wenye bashasha, na ninatumia maneno mazuri ya kumkaribisha.
7- Ninamkalisha mgeni mahala pazuri.
8- Ninamkirimu kwa ugeni wake, katika chakula na vinywaji.

Swali: 8- Eleza adabu za ugonjwa na za kuwatembelea wagonjwa?.

Jawabu: 1- Ninapohisi maumivu; ninaweka mkono wangu wa kulia sehemu inayouma, na ninasema: "Bismillaah" Mara tatu, na ninasema: "Audhu bi izzatillaahi waquduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhir" Mara saba, yaani: Ninajilinda kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari za yale ninayoyapata na ninachukua hadhari.
2- Ninaridhika na yale aliyoyakadiria na Mwenyezi Mungu na ninasubiri.
3- Ninafanya haraka kumtembelea ndugu yangu akiwa mgonjwa, na ninamuombea dua, na wala sikai kwake muda mrefu.
4- Ninamfanyia kisomo bila ya yeye kuniomba.
5- Ninamuhusia kuvumilia, kuomba dua, kuswali, na kuwa twahara kwa kadiri awezavyo.
6- Dua ya mgonjwa: "As alullaahal Adhwiim Rabbal Arshil Adhwiim an yash-fiyaka" Mara saba, Yaani: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu akuponye.

Swali: 9- Eleza adabu za kutafuta elimu?

Jawabu: 1- Kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka.
2- Naifanyia kazi elimu niliyojifunza.
3- Namuheshimu mwalimu na ninampa daraja yake anapokuwepo na anapokuwa hayupo.
4- Nakaa mbele yake kwa adabu.
5- Nanyamaza na kumsikiliza vizuri, na wala simkatishi katika somo lake.
6- Ninakuwa na adabu ninapouliza swali.
7- Simuiti kwa jina lake.

Swali: 10- Ni zipi adabu za vikao?.

Jawabu: 1- Nawasalimia walioko katika kikao.
2- Na ninakaa pale kinapoishia kikao, simnyanyui yeyote mahali alipokaa wala sikai kati ya watu wawili isipokuwa kwa idhini yao.
3- Ninaacha nafasi katika kikao ili akae mtu mwingine.
4- Sikatishi mazungumzo ya kikao.
5- Ninaomba idhini na ninatoa salamu kabla ya kuondoka katika kikao.
6- Kinapomalizika kikao ninaomba dua ya kafara ya kikao. Sub-haanakallaahumma, wabihamdika, Ash-hadu an laa ilaaha illaa anta, Astaghfiruka wa atuubu ilaika, maana yake " Umetakasika ewe Mwezi mungu, na sifa njema ni zako, nashuhudia kuwa hakuna mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa ni wewe, ninakuomba msamaha na ninatubia kwako).

Swali: 11- Eleza adabu za kulala.

Jawabu: 1- Nalala mapema.
2- Nalala na twahara.
3- Silalii tumbo.
4- Ninalalia ubavu wangu wa kulia, na ninaweka mkono wangu wa kulia chini ya shavu langu la kulia.
5- Ninakung'unta na kutandika kitanda changu.
6- Ninasoma nyiradi za kulala, kuanzia ayatul kursiy, suratul ikhlaswi, na sura za kinga mbili (Suratul falaq na suratun nas) mara tatu tatu, na ninasema: "Bismikallaahumma amuutu wa ahya" Yaani: Kwa jina lako Mola wangu ninakufa, na ninakuwa hai.
7- Naamka kwa ajili ya swala ya alfajiri.
8- Na ninasema baada ya kuamka kutoka usingizini: "Alhamdulillaahi lladhi ah-yaanaa baada maa amaatanaa wailaihin nushuur" Yaani: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyetuhuisha baada ya kutufisha na kwake tutafufuliwa.

Swali: 12- Ni zipi adabu za chakula?.

Jawabu:
1- Ninanuia kwa kula kwangu na kunywa kwangu nipate nguvu ya kumtii Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
2- Kuosha mikono miwili kabla ya kula.
3- Ninasema: "Bismillah", Na ninakula kwa mkono wangu wa kulia na kwa chakula kilicho mbele yangu, na wala sili katikati ya sahani, au mbele ya mwenzangu.
4- Nikisahau bismillah ninasema: "Bismillahi awwaluhu wa aakhiruhu", kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho wake.
5- Ninaridhika na chakula kinachopatikana, na wala sikitoi dosari chakula, kinaponifurahisha nakula, na kisiponifurahisha nakiacha.
6- Ninakula matonge kadhaa tu, na wala sili sana.
7- Na wala sipulizi chakula au kinywaji, na ninakiacha mpaka kipoe.
8- Ninakaa pamoja na watu wengine kwenye chakula, pamoja na familia au mgeni.
9- Sianzi kula chakula kabla ya wenzangu ambao ni wakubwa kuliko mimi.
10- Ninamtaja Mwenyezi Mungu wakati ninapokunywa, na ninakunywa nikiwa nimekaa kwa mafundo matatu.
11- Ninamshukuru Mwenyezi Mungu wakati ninapomaliza kula.

Swali: 13- Orodhesha adabu za kuvaa?

Jawabu: 1- Ninaanza kuvaa nguo yangu kuanzia kulia, na ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo.
2- Sirefushi nguo yangu mpaka chini ya kongo mbili za miguu.
3- Hawavai watoto wa kiume nguo za watoto wa kike, wala wa kike nguo za kiume.
4- Kutokujifananisha na mavazi ya makafiri au watu waovu kama wasanii.
5- Kusema bismillah wakati wa kuvua nguo.
6- Kuvaa kiatu cha kulia kwanza, na kuvua kuanzia kushoto.

Swali: 14- Eleza adabu za kupanda kiando?

Jawabu: 1- Ninasema: "Bismillah, Ahamdulillaah", «Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyetudhalilishia (kipando) hiki, na hatukuwa ni wenye uwezo juu yake.» «Na sisi baada ya kufa kwetu ni wenye kuelekea Kwake na kurejea." [Suratuz zukhruf: 13,14].
2- Ninapopita kwa muislamu; ninamtolea salamu.

Swali: 15- Eleza adabu za njia.

Jawabu: 1- Ninatembea sawa na ninakuwa mnyenyekevu wakati wa kutembea, na ninatembelea upande wa kulia wa njia.
2- Ninamtolea salamu ninayekutananaye.
3- Ninainamisha macho yangu na wala simuudhi yeyote.
4- Ninaamrisha Mema Na Kukataza Mabaya:
5- Ninaondoa udhia njiani.

Swali: 16- Eleza Adabu za kuingia nyumbani na za kutoka:

Jawabu: 1- Ninatoka kwa mguu wangu wa kushoto na ninasema: (Kwa jina la Mwenyezi Mungu,nimemtegemea kwa Mwenyezi Mungu na hakuna hila (namna) wala nguvu isipokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Ewe Mola wangu wa haki hakika mimi najikinga kwako ili nisipotee au kupotezwa au kuteleza na kufanyakosa au kutelezeshwa na kufanya makosa au kudhulumu au kudhulumiwa au kudanganya au kudanganywa mimi) 2- Ninaingia ndani kwa mguu wangu wa kulia, na ninasema: "Bismillah walajinaa, wabismillahi kharajinaa, wa a'laa Rabbinaa tawakkalna" Kwa jina la Mwenyezi Mungu tumerejea, na kwa jina la Mwenyezi Mungu tulitoka, na kwa Mola wetu ndiko tunako tegemea.
3- Naaanza kuswaki kisha ninawasalimia walioko nyumbani.

Swali: 17- Eleza adabu za kukidhi haja.

Jawabu: 1- Ninaingia kwa mguu wangu wa kushoto.
2- Na ninasema kabla ya kuingia: Allaahumma inni audhubika minal khubuthi wal khabaa ithi": "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike."
3- Singii kitu chochote ambacho ndani yake ametajwa Mwenyezi Mungu.
4- Ninajisitiri wakati wa kukidhi haja.
5- Sizungumzi sehemu ya kukidhi haja.
6- Sielekei kibla, na wala sikipi mgongo wakati wa kukidhi haja ndogo au kubwa.
7- Ninatumia mkono wangu wa kushoto katika kuondoa najisi, na wala situmii mkono wa kulia.
8- Sikidhi haja yangu katika njia ya watu au kivuli chao.
9- Ninaosha mkono wangu baada ya kukidhi haja.
10- Ninatoka kwa mguu wangu wa kushoto na ninasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.

Swali: 18- Eleza adabu za msikiti.

Jawabu: 1- Ninaingia msikitini kwa mguu wangu wa kulia, na ninasema: "Bismillaah, Allahummaftah li Abwaba rahmatika" Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Ewe Mola nifungulie milango ya rehema zako.
2- Sikai mpaka niswali rakaa mbili.
3- Sipiti mbele ya mwenye kuswali, au kutangaza kilichopotea msikitini, au kuuza au kununua msikitini.
4- Ninatoka msikitini kwa mguu wangu wa kushoto, na ninasema: "Allahumma inni as aluka minfadhlika". Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe katika fadhila zako.

Swali: 19- Eleza adabu za salamu.

Jawabu: 1- Ninapokutana na muislamu naanza kumsalimia, kwa kauli: "Assalaamu alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh" wala siachi kutoa salamu, na wala simuashirii kwa mkono pekee.
2- Ninatabasamu katika uso wa ninayemsalimia.
3- Ninampa mkono wangu wa kulia.
4- Anaponisalimia yeyote kwa salamu ninamjibu kwa uzuri zaidi kuliko alivyonisalimia, au ninamjibu kwa mfano wa alivyosalimia.
5- Simuanzi kafiri kwa salamu, na akinisalimia ninamjibu kama alivyonisalimia.
6- Na mdogo anamsalimia mkubwa, na aliyepanda anamsalimia mtembea kwa miguu, na mtembea kwa miguu anamsalimia aliyekaa, na wachache wanawasalimia wengi.

Swali: 20 Ni zipi adabu za kuomba ruhusa?

Jawabu: 1- Ninaomba idhini kabla ya kuingia mahali.
2- Ninaomba idhini mara tatu na wala sizidishi, na baada ya hapo ninaondoka.
3- Ninagonga mlango taratibu, na wala sisimami mbele ya mlango, bali nasimama kuliani kwake au kushotoni kwake.
4- Singii kwa baba yangu na mama yangu au chumba chochote kabla ya kuomba idhini, na hasa hasa kabla ya alfajiri na wakati wa kupumzika mchana (Qailula), na baada ya swala ya ishaa.
5- Ninaweza kuingia sehemu zisizoishi watu, mfano kama Hospitali au majumba ya biashara bila kuomba idhini.

Swali: 21- Eeleza adabu za kuwahurumia wanyama?

Jawabu: 1- Ninawalisha wanyama na ninawanywesha.
2- Kuwahurumia, kuwafanyia upole wanyama, na kutokuwabebesha mizigo wasiyoiweza.
3- Siwaadhibu wanyama kwa aina yoyote ya adhabu na maudhi.

Swali: 22- Eleza adabu za michezo:

Jawabu: 1- Ninanuia kwa michezo hii kupata nguvu kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu na kumridhisha.
2- Hatuchezi wakati wa swala.
3- Watoto wa kiume hawachezi na watoto wa kike.
4- Ninavaa mavazi ya michezo yenye kusitiri uchi.
5- Ninajiepusha na michezo iliyoharamishwa, kama ambayo ndani yake kuna kupiga uso na kufunua uchi.

Swali: Eleza baadhi ya adabu za mizaha.

Jawabu: 1- Ukweli katika mizaha na kutokuwa muongo.
2- Mizaha iliyoepukana na kejeli, kudhihaki, kumuudhi mtu na kumtisha.
3- Kutokuzidisha mizaha.

Swali: 24- Eleza adabu za kupiga chafya.

Jawabu: 1- Kuweka mkono au nguo au kitambaa wakati wa kupiga chafya.
2- Kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kupiga chafya kwa kusema: "Alhamdulilllah"
3- Na aliyemsikia aseme kumwambia ndugu yake: "Yar-hamukallaah" Mwenyezi Mungu akuhurumie.
Akisema kumwambia hivyo:
Basi naye aseme: "Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum" Akuongozeni Mwenyezi Mungu na akutengenezeeni mambo yenu".

Swali: 25- Ni zipi adabu za kupiga mwayo?.

Jawabu: 1- Kujitahidi kuzuia mwayo.
2- Kutonyanyua sauti kwa kusema: "Aaah" Aaah".
3- Kuweka mkono juu ya mdomo.

Swali: 26- Eleza adabu za kusoma.

Jawabu: 1- Kusoma nikiwa na twahara baada ya kutia udhu.
2- Kukaa kwa adabu na heshima.
3- Ninaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani mwanzo wa kusoma.
4- Ninazingatia kisomo.

Sehemu ya tabia:30

Swali: 1- Eleza fadhila za tabia njema.

Jawabu: Amesema Mtume Sala na amani ziwe juu yake: "Muumini aliyekamilika kiimani ni yule mwenye tabia njema zaidi kuliko wengine". Kaipokea Tirmidhiy na Ahmad.

Swali: 2- Kwa nini tunashikamana na tabia za kiislamu.

Jawabu: 1- Kwa sababu ni sababu ya kumpenda ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
2- Ni sababu ya kupendwa na viumbe.
3- Ni kitu kizito zaidi katika mizani.
4- Na malipo huzidishwa kwa sababu ya tabia njema.
5- Ni alama ya ukamilifu wa imani.

Swali: 3- Ni wapi tunachukua tabia njema?.

Jawabu: Kutoka katika Qur'ani tukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye yale yaliyo nyooka kabisa}. [Suratul Israai: 9]. Na kutoka katika mafundisho ya Mtume: amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hakika bila shaka nimetumwa ili nitimilize tabia njema". Imepokelewa na Ahmad.

Swali: 4- Ni zipi tabia za wema na namna zake?

Jawabu: Wema: Ni kumchunga Mwenyezi Mungu wakati wote, na kufanya mambo mazuri na kuwafanyia wema viumbe.
Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu ameandika wema juu ya kila kitu". Imepokelewa na Imamu Muslim
Miongoni mwa namna za wema:

Ni kufanya wema zaidi katika ibada za Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na hilo linakuwa kwa kutakasa nia katika ibada zake.
-Kuwafanyia wema wazazi wawili, kwa kauli na vitendo.
-Kuwafanyia wema ndugu wa kuzaliwa tumbo moja na wale wa karibu katika ukoo.
-Kumfanyia wema jirani.
-Kuwafanyia wema mayatima na masikini.
-Kumfanyia wema aliyekukosea.
-Kufanya wema katika mazungumzo.
-Kufanya wema katika mijadala.
-Kumfanyia wema mnyama.

Swali: 5- Ni kipi kinyume cha wema?

Jawabu: kinyume cha wema ni kukosea (kukwaza).
Miongoni mwa makosa:
Ni kuacha kutakasa nia katika ibada za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na kuwaasi wazazi wawili.
Kukata undugu.
Kuishi vibaya na majirani.
Kuacha kuwafanyia wema mayatima na masikini, na mengineyo katika aina za mazungumzo na matendo mabaya.

Swali: 6- Ni zipi aina za amana na namna zake?.

Jawabu:
1- Amana katika kuhifadhi haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Aina zake:
Amana katika utekelezaji wa ibada kama swala, zaka, swaumu, Hijja, na zinginezo katika zile alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu juu yetu.
2- Amana katika kuhifadhi haki za viumbe:
Ikiwemo kuhifadhi heshima za watu.
Na mali zao.
Na damu zao.
Na siri zao, na yote ambayo watu wamekuamini.
Amesema Mwenyezi Mungu katika kutaja sifa za waliofaulu:
"Na wale ambao wanavitunza vitu vyote walivyoaminiwa navyo, na wanatekeleza ahadi zao zote." [Suratul Mu'minun: 8]

Swali: 7- Ni kipi kinyume cha amana?

Jawabu: Ni hiyana, nayo maana yake ni kupoteza haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za watu.
Amesema Mtume Sala na amani ziwe juu yake:
"Alama za mnafiki ni tatu" Na akataja miongoni mwa hizo alaama "Na akiaminiwa anafanya hiyana" Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 8- Ni ipi tabia ya ukweli?

Jawabu: Ni kueleza kwa namna inayoendana na uhalisia wa tukio au kukieleza kitu kama kilivyo.
Na katika namna zake:

Ukweli wakati wa mazungumzo na watu.
Ukweli katika ahadi.
Ukweli katika kila kauli na kitendo.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake:
"Hakika ukweli unamuongoza mtu katika wema, na hakika wema unamuongoza mtu katika pepo, na hakika mtu husema kweli mpaka anakuwa mkweli" Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 9- Ni kipi kinyume cha ukweli?

Jawabu: Ni uongo, nao ni kinyume cha uhakika, na miongoni mwake, ni kuwaongopea watu, kutotimiza ahadi, na kutoa ushahidi wa uongo.
Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Na Tahadharini sana na uongo! kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu unampelekea mtu kuingia Motoni, na hatoacha mtu kuendelea kusema uongo, na kuutafuta uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo". Wamekubaliana Bukhari na Muslim. Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Alama za mnafiki ni tatu" Na akataja miongoni mwake "Akizungumza husema uongo, na akitoa ahadi hatimizi". Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 10- Eleza aina za subira.

Jawabu: Kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kusubiri kutoyaendea maasi.
-kusubiri juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu yaumizayo, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila hali.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kusubiri" [Surat Al Imrani: 146] Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini: akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake." Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 11- Ni kipi kinyume cha subira?

Jawabu: Ni kutokuvumilia juu ya kumtii Mwenyezi Mungu, kutosubiri katika kuyaendea maasi, kulalamika na kuchukia makadirio kwa kuzungumza au vitendo vinavyoonyesha kutoridhishwa na makadirio.
Katika namna zake:

Kutamani kifo.
Kupiga mashavu.
Kuchana nguo.
Kusambaza nywele, kwa itikadi za kutoridhishwa na msiba uliotokea.
Kujiombea maangamivu.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake:
"Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu)." Kaipokea Tirmidhi na bin Majah

Swali: 12- Eleza tabia ya kusaidizana.

Jawabu: Ni watu kusaidizana wao kwa wao katika haki na mambo ya kheri.
Namna za kusaidizana:

* Kusaidizana katika kurudisha haki za watu.
* Kusaidizana katika kumzuia mwenye kudhulumu.
* Kusaidizana katika kukidhi mahitaji ya watu na masikini.
* Kusaidina katika kila kheri.
* Kutosaidizana katika madhambi na maudhi na uadui.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na saidianeni katika wema na uchamungu na wala msisaidiane katika madhambi na kufanya uovu,na muogopeni Mwenyezi Mungu kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu" [Suratul Maidah: 2] Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Muumini kwa muumini mwenzake ni kama jengo moja; linajiimarisha baadhi yake kwa baadhi" Wamekubaliana Bukhari na Muslim. Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Muislamu ndugu yake ni muislamu, asimdhulumu na wala asimsaliti, na atakayekuwa katika shida ya ndugu yake, basi Mwenyezi Mungu naye atakuwa katika shida yake, na atakayetatua kwa muislamu matatizo, basi na Mwenyezi Mungu atamtatulia tatizo katika matatizo ya siku ya kiyama, na atakayemsitiri muislamu, Mwenyezi Mungu naye atamsitiri siku ya kiyama". Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 13- Ni zipi aina za tabia ya haya (Aibu)?

Jawabu: 1- Kumuonea haya Mwenyezi Mungu: inakuwa kutomuasi mwenyezi mungu Mtukufu.
2- Kuwaonea haya watu: Na miongoni mwa haya ni kuacha maneno mabaya machafu, na kufunua uchi.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Imani iko zaidi ya sehemu sabini". "Au zaidi ya sitini" sehemu ya juu yake zaidi ni kauli ya (Laa ilaaha illa llaahu) Hapana Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ya chini yake zaidi ni kuondoa maudhi njiani, na haya (aibu) ni sehemu katika imani." Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 14- Eleza namna za tabia ya huruma.

Jawabu: -Kuwahurumia wazee na kuwaheshimu.
- Kuwahurumia wadogo na watoto.
- Kumhurumia masikini na mwenye shida.
-Kuwahurumia wanyama kwa kuwalisha na kutowaudhi.
Na katika hili ni kauli ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake:
"Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu" Wamekubaliana Bukhari na Muslim. Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni watu wa ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni." Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy.

Swali: 15- Ni zipi aina za tabia ya mapenzi?

Jawabu: Ni kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na wale walioamini wanamapenzi makubwa kwa Mwenyezi Mungu" [Suratul Baqara: 165].
Kumpenda mtume - rehema na amani ziwe juu yake
Amesema:
"Namuapia yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake zaidi kuliko mtoto wake na mzazi wake". Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kuwapenda waumini, na kuwapendelea kheri kwao kama unavyoipendelea nafsi yako.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake:
"Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake" Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Swali: 16- Eleza nini maana ya bashasha?

Jawabu: Ni ukunjufu wa uso, pamoja na furaha, tabasamu, upole na kudhihirisha furaha wakati wa kukutana na watu.
Nayo ni kinyume cha kukunja sura mbele za watu, kitu kinachoweza kuwafanya wakawanaye mbali.
Na katika faida zake, zimekuja hadithi nyingi, Kutoka kwa Abuu Dhari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: alisema kuniambia mimi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Usidharau kabisa katika wema kitu chochote, hata kama ni kukutana na ndugu yako kwa uso mkunjufu." Imepokelewa na Imamu Muslim Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Tabasamu lako katika uso wa ndugu yako ni sadaka" Kaipokea Imamu Tirmidhiy

Swali: 17- Husuda ni nini?

Jawabu: Ni kutamani neema ziwaondokee wengine, au kuchukia neema walizo pewa mtu.
Amesema Mtukufu:
"(Na ninaomba kinga kutokana) Na shari ya hasidi anapofanya husuda" [Suratul Falaq: 5]
Na Kutoka kwa Anasi bin Maliki Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake amesema: "Msichukiane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, nakuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja" Ameipokea Bukhari na Muslim.

Jawabu: 18- Nini maana ya masihara?

Jawabu: Ni kumfanyia kejeli ndugu yako muislamu na kumdharau, na jambo hili halifai.
Amesema Mtukufu katika kulikemea hilo:
"Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo, wasitoke Waumini wanaume wakawacheza shere Waumini wanaume wengine, huenda akawa yule anayechezwa shere katika wao ni bora kuliko wale wenye kucheza shere, na wasitoke Waumini wa kike wakawacheza shere Waumini wakike wengine, kwani huenda yule anayechezwa shere miongoni mwao ni bora kuliko wale wenye kucheza shere. Wala msitiane dosari nyinyi kwa nyinyi, wala msiitane majina ambayo yanachukiwa na wenye kuitwa nayo, kwani ubaya wa sifa na jina ni utokaji nje ya maadili ya Dini, nao ni kucheza shere kwa njia ya dharau, kuaibisha kwa maneno au ishara na kupeana majina mabaya, baada ya kuwa mmeingia kwenye Uislamu na mmeufahamu. Na Asiyetubia na huku kuchezeana shere, kutiana dosari, na kuitana majina mabaya na utokaji nje wa maadili ya Dini, basi hao ndio watu waliozidhulumu nafsi zao kwa kuyatenda mambo haya yaliyokatazwa." [Suratul Hujurat: 11].

Swali: 19- Elezea unyenyekevu ni nini?

Jawabu: Ni mtu kutojiona yeye ni bora kwa watu, akawa hawadharau watu na wala haikatai haki.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na waja wa Arrahman mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha" [Suratul Furqan: 63], Yaani: Wakiwa wanyenyekevu. -Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Na hajawahi kunyenyekea yeyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua" Imepokelewa na Imamu Muslim Na amesema Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu ameteremsha wahyi kwangu, yakuwa kuweni wanyenyekevu kiasi kwamba asifanye uovu mmoja wenu kwa mwingine, na asichupe mipaka mmoja wenu juu ya mwingine". Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 20-Ni zipi aina za kiburi kilicho haramishwa?

Jawabu: 1- Kufanya kiburi katika haki, nacho ni kuikataa haki na kutokuikubali.
2- Kuwafanyia kiburi watu, nako ni kuwadharau na kuwabeza.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Haingii peponi atakayekuwa moyoni mwake na chembe ndogo ya kiburi" Mtu mmoja akasema: Kuna mtu anapenda nguo yake kuwa nzuri, na viatu vyake kuwa vizuri (pia ni kiburi?) Akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri anapenda uzuri, kiburi: Ni kuikataa haki na kuwadharau watu" Imepokelewa na Imamu Muslim
-Kuibeza haki: Kuikataa.
-Kuwadharau watu: kuwabeza.
- Nguo nzuri na viatu vizuri hivi si katika kiburi.

Swali: 21- Taja aina za baadhi ya udanganyifu iliyoharamishwa.

Jawabu: Udanganyifu katika kuuza na kununua, nako ni kuficha aibu ya bidhaa.
-Udanganyifu katika kujifunza elimu, na mfano wake ni ghushi ya wanafunzi katika mitihani.
-Udanganyifu katika kauli kama kushuhudia uongo na kusema uongo.
- Kutotimiza unayoyasema na yale unayokubaliana na watu.
Na katika katazo la kudanganya, yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alipita katika gunia la chakula, akaingiza mkono wake ndani yake, vidole vyake vikapata unyevunyevu, akasema: "Ni nini hiki ewe muuza chakula?" Akasema: Kimenyeshewa na mvua ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema: "Kwa nini usikiweke juu ili watu wakione? Yeyote mwenye kudanganya si miongoni mwangu" Imepokelewa na Imamu Muslim
Gunia: Ni mfuko wa chakula.

Swali: 22- Kusengenya ni nini?

Jawabu: Ni kumsema ndugu yako muislamu kwa yale anayoyachukia akiwa hayupo katika mazungumzo.
Alisema Allah Mtukufu:
"Na wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi, Je yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo (bila shaka) Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea toba, mwenye kurehemu" [Suratul Hujurat: 12].

Swali: 23- Elezea maana ya umbea.

Jawabu: Ni kuhamisha mazungumzo kati ya watu kwa ajili ya kuwavuruga.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Haingii peponi mfitinishaji" Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 24- Uvivu ni nini?

Jawabu: Ni kuwa mzito katika kufanya mambo ya kheri na yale ambayo ni ya wajibu kwa mtu kuyafanya.
Na katika hayo ni kuwa mvivu katika kutekeleza majukumu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Hakika mbinu ya wanafiki hawa ni kumhadaa Mwenyezi Mungu kwa Imani wanayojionyesha nayo na ukafiri wanaouficha, kwa kudhani kuwa mbinu yao itafichikana kwa Mwenyezi Mungu, na hali ya kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Anayewahadaa na ni Mwenye kuwalipa malipo yanayofanana na vitendo vyao. Wanafiki hawa wanaposimama kutekeleza Swala, wanasimama kufanya hivyo kwa uvivu, wanakusudia, kwa kuswali kwao, kuonekana na kusikika. Na wao hawamtaji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, isipokuwa kumtaja kwa uchache". [Suratun Nisaa: 142]
Ni lazima kwa muumini kuacha uvivu, kuzubaa na kukaa, na aende mbio katika amali na achangamke na afanye bidii na juhudi katika maisha haya kwa yale yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Swali: 25- Eleza aina za hasira?

Jawabu: 1- Hasira nzuri: Nayo ni ile inayokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pale makafiri au wanafiki au wengineo wanapoyaendea maharamisho yake Mtukufu.
2- Hasira mbaya: Nayo ni hasira inayompelekea mtu kufanya au kuzungumza mambo yasiyofaa.
TIBA YA HASIRA MBAYA:

Udhu - kutawadha.
Kukaa ikiwa atakuwa kasimama, na kulala ikiwa atakuwa amekaa.
Ashikamane na usia wa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika hilo:
"Usikasirike"
Aidhibiti nafsi kutosukumwa na hasira akafanya maamuzi mabaya.
Kujikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa
Kunyamaza.

Swali: 26- Nini maana ya kupeleleza?

Jawabu: Ni kubaini na kutafuta aibu za watu pamoja na yale waliyoyasitiri.
Miongoni mwa aina zake za haramu:

- Kuchungulia uchi wa watu majumbani.
-Mtu kusikiliza mazungumzo ya watu bila ya wao kujua.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na wala msichunguzane". [Suratul Hujurat: 12].

Swali: 27- Nini maana ya ubadhirifu? (ufujaji) Na nini maana ubahili? Na ukarimu ni nini?

Jawabu: Ubadhirifu: Ni kutumia mali bila sababu za msingi.
Na kinyume chake:
Ni Ubahili: Nako ni kuzuia kutoa katika jambo la lazima.
Na sahihi zaidi nikuwa katikati ya hayo, na muislamu anatakiwa kuwa mkarimu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na wale ambao wakitumia mali zao hawapitishi kipimo katika kutoa wala hawabani katika matumizi, na kutumia kwao huwa kuko kati na kati baina ya kupitisha kipimo na kubana." [Suratul Furqan: 67],

Swali: 28- Uoga ni nini? Na ushujaa ni nini?

Jawabu: Uoga: Ni mtu kuogopa kitu ambacho hakitakiwa kuogopwa.
Mfano:
Kuogopa kusema ukweli na kukemea uovu.
Ushujaa:
Ni kujitosa katika ukweli, nao ni kama mfano wa kwenda mbele katika viwanja vya vita kwa ajili ya kuutetea uislamu na waislamu.
Na alikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akisema katika dua yake:
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na uoga". Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Allah kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri" Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 29- Taja baadhi ya maneno ya ulimi yaliyoharamishwa.

Jawabu: Mfano kutoa laana na kutukana.
- Na mfano ni kauli ya fulani "We hayawani" Au mfano wake katika matamshi.
- Au kutaja nyuchi katika maneno mabaya na machafu.
- Na aliyakataza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake hayo yote, akasema: "Muumini si msemaji watu vibaya, wala mtoaji wa laana, wala muovu, wala mwenye kauli chafu" Kaipokea Tirmidhi na bin Majah.

Swali: 30- Eleza sababu zinazoweza kumsaidia muislamu kufikia katika tabia njema?.

Jawabu: 1- Kumuomba Mwenyezi Mungu amruzuku tabia njema na amsaidie juu ya hilo.
2- Kumchunga Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka, na kujua kuwa yeye anakujua, anakusikia na anakuona.
3- Kumbuka malipo ya tabia njema ni sababu ya kuingia peponi.
4- Kumbuka mwisho wa tabia mbaya, ni sababu ya kuingia motoni.
5- Kwamba tabia njema huleta mapenzi ya Mwenyezi Mungu na mapenzi ya viumbe wake, na tabia mbaya huleta ghadhabu za Mwenyezi Mungu na chuki za viumbe wake.
6- Kusoma historia ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake na kumuiga.
7- Kuambatana na watu wema na kujiepusha na kuambatana na watu waovu.

Sehemu ya Dua na Dhikri mbali mbali.43

Swali: 3- Ni upi ubora wa dhikiri?

Jawabu: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake ni mfano wa aliyehai na aliyekufa" Imepokelewa na Al-Bukhaariy
-Hii ni kwa sababu thamani ya maisha ya mtu huwa kulingana na kiwango chake cha kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Swali: 2- Eleza baadhi ya faida za kumtaja Mwenyezi Mungu.

Jawabu: 1- Humridhisha Arrahman -Mwingi wa rehema-.
2- Humfukuza shetani.
3- Humkinga muislamu kutokana na shari.
4- Hupatikana malipo na thawabu.

Swali: 3- Ni ipi dhikiri bora?

Jawabu: "Laa ilaaha illa llaahu" Hapana Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu. Kaipokea Tirmidhi na bin Majah.

Swali: 4- Unasema nini wakati wa kuamka kutoka usingizini?

"Al-hamdulillaahi lladhi ah-yaanaa baada maa amaatanaa wailaihin nushuur" Yaani: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyetuhuisha baada ya kutufisha na kwake tutafufuliwa. Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 5- Unasema nini unapovaa nguo yako?

Jawabu: "Alhamdulillaahil ladhi kasaani haadhath thauba warazaqaniihi min ghairi haulin minni walaa quwwatin". Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenivisha nguo hii na akaniruzuku si kwa ujanja wangu wala si kwa nguvu yangu" Imepokelewa na Abuu Daud na Tirmidhiy na wengineo.

Swali: 6- Una sema nini unapovua nguo?

Jawabu: "Bismillahi" Kaipokea Imamu Tirmidhiy

Swali: 7- Ni ipi dua ya kuvaa nguo mpya?

Jawabu: "Allaahumma lakal hamdu anta kasautanihi, as aluka khairahu wa khaira maa suni'a lahu, wa audhubika min sharrihi wa sharri maa suni'a lahu" Ewe Mwenyezi Mungu ni zako kila sifa njema, wewe ndiye uliyenivisha nguo hii, ninakuomba mazuri yake na mazuri iliyotengenezewa, na ninajilinda kwako kutokana na shari zake na shari ilizotengenezewa" Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy.

Swali: 8- Ni ipi dua ya kumuombea aliyevaa nguo mpya?

Jawabu: Utakapoona nguo mpya kwa mwenzako basi unamuombea, na unasema: "Utaimaliza na Allah Mtukufu atakupa badala" Imepokelewa na Abuu Daud

Swali: 9- Eleza dua ya kuingia chooni, nako ni mahali pa kukidhi haja.

"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike". Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 10- Ni ipi dua ya kutoka chooni?

"Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako. Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy.

Swali: 11- Unasema nini kabla ya udhu?

Jawabu: "Bismillahi" Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy na wengineo.

Swali: 12- Ni ipi dua baada ya kumaliza udhu?

"Nina shuhudia kuwa hapana Mola anastahiki kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake hana mshirika, na nina shuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na ni mtume wake". Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 13- Na ni ipi dua wakati wa kutoka nyumbani?

Jawabu: "Bismillaahi, tawakkaltu alallaahi, walaa haulaa walaa quwwata illaa billah" (Ninatoka) Kwa jina la Mwenyezi Mungu nimemtegemea Mwenyezi Mungu, na wala hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy.

Swali: 14- Ni ipi dua wakati wa kuingia nyumbani?

"Bismillah walajinaa, wabismillahi kharajinaa, wa a'laa Rabbinaa tawakkalna" Kwa jina la Mwenyezi Mungu tumerejea, na kwa jina la Mwenyezi Mungu tulitoka, na kwa Mola wetu ndiko tunako tegemea, kisha anawasalimia waliopo ndani. Imepokelewa na Abuu Daud

Swali: 15- Ni ipi dua ya kuingia msikitini?

Jawabu: "Allahummaftahli Ab-waba rahmatika"" Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako. Kaipokea Muslim.

Swali: 16- Eleza dua ya kutoka msikitini.

Jawabu: "Allaahumma inni as-aluka min fadhlika" Ewe Mwenyezi Mungu ninakuomba katika fadhila zako. Kaipokea Muslim.

Swali: 17- Unasema nini unaposikia adhana?

Jawabu: Ninasema kama anavyosema muadhini, isipokuwa katika neno: "Hayya a'las swalaa" na "Hayya a'lal falaah" Ninasema: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah" Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 18- Unasema nini baada ya adhana?

Jawabu: Ninamtakia rehema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-. Imepokelewa na Imamu Muslim Na ninasema: "Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah". Ewe Mwenyezi Mungu huu ni wito uliotimia, na swala imewadia, mpe Muhammadi wasiila (daraja) na nafasi, na umfufue nafasi nzuri uliyomuahidi. Kaipokea Bukhari.
Na ninaomba dua kati ya adhana na iqaama, kwani dua wakati huo hairejeshwi.

Swali: 19- Unasema nini asubuhi na jioni katika adhkari?.

Jawabu: 1- Ninasoma ayatul kursiy: (Itazame katika msahafu) "Mwenyezi Mungu Ndiye Ambaye hakuna yeyote anayestahiki uungu na kuabudiwa isipokuwa Yeye. Ndiye Aliye hai Ambaye Amekusanya maana yote ya uhai mkamilifu unaolingana na utukufu Wake. Ndiye Msimamizi wa kila kitu. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Kila kilichoko kwenye mbingu na kilichoko kwenye ardhi ni milki Yake. Na hatajasiri mtu yeyote kuombea mbele Yake isipokuwa kwa ruhusa Yake. Ujuzi Wake umevizunguka vitu vyote vilivyopita, vilivyoko na vitakavyo kuja. Anajua yaliyo mbele ya viumbe katika mambo ambayo yatakuja na yaliyo nyuma yao katika mambo yaliyopita. Na hakuna yeyote, katika viumbe, mwenye kuchungulia chochote katika elimu Yake isipokuwa kadiri ile ambayo Mwenyezi Mungu Amemjulisha na kumuonyesha. Kursiy Yake imeenea kwenye mbingu na ardhi. Kursiy ni mahali pa nyayo za Mola, uliyo mkubwa utukufu Wake, na hakuna ajuwaye namna ilivyo isipokuwa ni Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. Wala hakumuelemei Mwenyezi Mungu Aliyetakata kuzitunza. (hizo mbingu na ardhi).Yeye Ndiye Aliye juu ya viumbe Vyake vyote, kwa dhati Yake na sifa Zake, Aliyekusanya sifa za utukufu na kiburi. Aya hii ni aya tukufu zaidi katika Qur’ani, na inaitwa Āyah al- Kursīy." [Suratul Baqara: 255]. 2- Na ninasoma: Bismillaahir rahmanir rahiim. "Sema, ewe Mtume, «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo." "Mwenyezi Mungu ndiye mkusudiwa" (2) «Hakuzaa wala hakuzaliwa" «Wala hakuna yeyote katika viumbe Vyake mwenye kufanana katika Majina Yake, Sifa Zake wala vitendo Vyake.» Mara tatu. "Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake." Sema «Najilinda kwa mola wa mapambazuko". «Kutokana na shari la viumbe na udhia wao" «Na shari ya usiku wenye giza jingi uingiapo na ujikitapo na shari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake." «Na shari ya wachawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga." «Na shari ya hasidi mwenye kuchukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Alizowaneemesha ziwaondokee.» Mara tatu. "Naanza kusoma Qur’an kwa jina la Mwenyezi Mungu nikiomba msaada Wake. «Allah» ni jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa baraka Mwenye kutukuka, Anayestahiki kuabudiwa na sio mwingine. Nalo ni jina mahsusi zaidi miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na haitwi kwa jina hili yeyote isipokuwa Yeye Aliyetakasika na sifa za upungufu. «Al-Raḥmān» Mwenye rehema nyingi Ambaye rehema Zake zimewanea viumbe vyote. «Al-Raḥīm» mwenye kuwarehemu Waumini. Na majina mawili haya, kati ya majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, yanakusanya uthibitishaji wa sifa ya urehemefu kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kama unavyonasibiana na haiba Yake." "Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu" "Mfalme wa watu" (2) "Mola wa watu" «Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu." «Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu." «Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.» Mara tatu. 3- "Allaahumma anta rabii Laa ilaaha illaa anta, khalaqtanii wa ana abduka, wa anaa a'laa 'ahdika wawa'dika mastatwa'tu, audhubika min sharri maa swana'tu, abuu u laka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambii faghfirlii fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Tafsiri yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ni mja wako, hakuna Mola isipokuwa wewe, umeniumba na mimi ni mja wako, na mimi niko ndani ya ahadi yako, na ahadi yako (ninafanya) kadiri niwezavyo, ninajilinda kwako kutokana na shari ya yale niliyoyafanya, nina kiri kwako kwa neema zako juu yangu, na nina kiri kwako dhambi zangu, nisamehe, kwani hakuna awezaye kusamehe madhambi ila wewe". Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Swali: 20- Unasema nini wakati wa kulala?

Jawabu: "Bismikallaahumma amuutu wa ahya" Yaani: Kwa jina lako Mola wangu ninakufa, na ninakuwa hai. Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 21- Unasema nini kabla ya kula chakula?

Jawabu: "Bismillahi"
Basi ukisahau kuisema mwanzoni mwake basi sema:
"Bismillaahi fii awwalihi wa aakhirihi" Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzoni mwake na mwishoni mwake. Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy.

Swali: 22- Unasema nini wakati wa kumaliza kula chakula?

Jawabu: "Alhamdulillaahil ladhi atwa'amanii hadhaa warazaqaniihi min ghairi haulin minni walaa quwwatin". Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki na akaniruzuku si kwa ujanja wangu wala si kwa nguvu yangu" Kaipokea Abuudaudi na bin Maajah na wengineo.

Swali: 23- Ni ipi dua ya mgeni kwa mwenyeji aliyemuandalia chakula?

Jawabu: "Allaahumma baarik lahum fii maa razaqtahum, waghfir lahum warhamhum" Ewe Mwenyezi Mungu wabariki katika vile ulivyowaruzuku, na uwasamehe na uwahurumie. Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 24- Anasema nini mtu anapopiga chafya?

Jawabu: "Alhamdulillaah" Hakika sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu.
3- Na ndugu yake aseme kumwambia ndugu yake: "Yar-hamukallaah" Akuhurumie Mwenyezi Mungu.
Akisema kumwambia hivyo:
Basi naye aseme: "Yah-diikumullaahu wayuslih baalakum" Akuongozeni Mwenyezi Mungu na akutengenezeeni mambo yenu". Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Swali: 25- Unasema nini wakati wa kumaliza kikao? "Dua ya kafara ya kikao?

"Sub-haanakallaahumma wabihamndika Ash-hadu an laa ilaaha illaa anta Astaghafiruka wa atuubu ilaika. Maana yake " Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu, Na sifa njema ni zako, ninashuhudia kuwa hapana Mola ila wewe, ninakuomba msamaha na ninatubia kwako. Imepokelewa na Abuu Daud na Tirmidhiy na wengineo.

Swali: 26- Ni ipi dua ya kupanda kipando?

Jawabu: Bismillaah Alhamdulillaah. "Sub-haanalladhi sakh khara lanaa haadhaa wamaa kunnaa lahu muqriniina, wa inna ilaa rabbinaa lamunqalibuun" Yaani: «Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyetudhalilishia (kipando) hiki, na hatukuwa ni wenye uwezo juu yake. Na hakika sisi kwa Mola wetu ni wenye kurejea» Alhamdulillaah, Alhamdulillaah, Alhamdulillaah, Allahu Akbaru Allahu Akbaru, Allahu Akbaru, Sub-haanaka llaahumma inni dhwalamtu nafsi faghfir li fa innahuu laa yaghfirudh dhunuuba illaa anta" Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nimeidhulumu nafsi yangu nisamehe, kwani hakika hakuna ewezaye kusamehe madhambi isipokuwa wewe. Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy.

Swali: 27- Eleza dua ya safari.

Jawabu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, Allahu Akbaru, "Sub-haanalladhi sakh khara lanaa haadhaa wamaa kunnaa lahu muqriniina, wa inna ilaa rabbinaa lamunqalibuun" Allaahumma inna nas aluka fii safarina haadhaa albirra wattaqwaa waminal amali maa tardhwaa, Allaahumma hawwin a'lainaa safaranaa haadhaa wat-wi anna bu'dahu, Allaahumma antas swaahibu fis safari, wal khaliifatu fil ahli, Allaahumma inni audhubika min wa'thaais safari, waka aabatil mandhwari, wasuuil munqalabi fil maali wal ahli" Maana yake: Mwenyezi Mungu mkubwa, Mwenyezi Mungu mkubwa, Mwenyezi Mungu mkubwa «Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyetudhalilishia (kipando) hiki, na hatukuwa ni wenye uwezo juu yake. Na hakika sisi kwa Mola wetu ni wenye kurejea» Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakuomba katika safari yetu hii wema na uchamungu, na katika amali zile unazoziridhia, ewe Mwenyezi Mungu turahisishie safari yetu hii na utupunguzie umbali wake, Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndiye rafiki katika safari, na ndiye msimamizi katika familia, Ewe Mwenyezi Mungu hakika najilinda kwako kutokana na uchovu wa safari, na mandhari mabaya, na kurejea kubaya katika mali na familia.
Na anaporejea basi atasema maneno hayo, na ataongeza neno:
"Aayibuun, taaibuun, aabiduun, lirabbinaa haamiduun" tumerejea, na tumetubia, na tunamuabudu Mwenyezi Mungu, na kwa Mola wetu ndiko tunakorejesha shukurani. Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 28- Ni ipi dua ya msafiri kwa mkazi?

Jawabu: "Astaudiukumullaahu lladhii laa tadhwiiu wadaa iu'hu" Maana yake: Nakukabidhini kwa Mwenyezi Mungu ambaye hakipotei alichokitunza. Kaipokea Ahmadi na bin Maaja.

Swali: 29- Ni ipi dua ya mkazi kwa msafiri?

Jawabu: "Astaudiullaaha diinaka, wa amaanataka, wa khawaatiima a'malaka" Maana yake: Ninamkabidhi Mwenyezi Mungu dini yako, na amana yako, na mwisho wa matendo yako. Ameipokea Ahmad na Al- nasaai.

Swali: 30- Ni ipi dua ya kuingia sokoni?

Jawabu: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul mulku walahul hamdu, yuhyii wa yumiitu, wahuwa hayyun laa yamuutu, biyadihil khairi, wahuwa a'laa kulla shai in qadiir" Maana yake: Hapana Mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika wake, ufalme ni wake na sifa njema ni zake, anahuisha na kufisha, mkononi mwake kuna kheri, naye juu ya kila kitu ni muweza. Kaipokea Tirmidhi na bin Majah

Swali: 31- Taja dua wakati wa hasira.

"A'udhubillaahi minash-shaitwanir rajiim" Maana yake: Ninajikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa. Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Swali: 32- Unasema nini kumwambia aliyekufanyia wema?

"Jazaakallaahu khairan" Allah akuzidishie kheri. Kaipokea Imamu Tirmidhiy

Swali: 33- Ni ipi dua ya kuomba kinapochoka kipando?

Jawabu: "Bismillahi" Imepokelewa na Abuu Daud

Swali: 34- Unasema nini likitokea jambo linalokufurahisha?

"Al-hamdulillaah lladhii bini'matihi tatimmus swaalihaat": Kila Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye kwa neema zake hutimia mambo mema. Ameipokea Al Hakim na wengineo.

Swali: Unasema nini yakitokea mambo yanayokuchukiza?

"Al-hamdulillaahi a'laa kulli haal" Kila Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu kwa kila hali Hadithi iko katika sahihil Jaamii.

Swali: 36- Ni ipi namna ya kutoa salamu na kuitika salamu?

Jawabu: Muislamu husema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatu" Maana yake: Amani iwe juu yenu na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake.
Na ndugu yake humjibu:
"Waalaikumussalaam warahmatullahi wabarakaatuh" Na iwe juu yenu Amani na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake. Ameipokea At-tirmidhiy na Abuu daawod na Ahmad.

Swali: 37- Ni ipi dua ya kusoma wakati wa kunyesha mvua?

"Allaahumma swayyiban naafi'a" (Ewe Mwenyezi Mungu ijaalie Mvua Hiyo ni yenye kupatia na yenye manufaa) Kaipokea Bukhari.

Swali: 38- Ni ipi dua ya kusoma baada ya kunyesha mvua?

Jawabu: "Mutwirnaa bifadhli llaahi warahmatihi" Tumenyeshelezewa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake. Kaipokea Bukhari na Muslim.

Swali: 39- Taja dua ya upepo mkali.

"Allahumma innii as aluka khairaha wa audhubika min sharri haa": Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba kheri zake na nina jikinga kwako nashari zake. Kaipokea Abuudaud na bin Maajah.

Swali: 40- Eleza dua unaposikia radi.

Jawabu: "Sub-haana lladhii yusabbihu rra'du bihamdihi wal Malaaikatu min khiifatihi" Maana yake: Ametakasika yule ambaye radi inamtakasa kwa kumhimidi na Malaika kwa kumuhofu. Muwattwaa Malik.

Swali: 41- Ni ipi dua ya kuomba unapomuona mwenye mtihani?

Jawabu: "Al-hamdulillaahi lladhii aafaani min mab-talaaka bihi, wafadh dhwalanii alaa kathiirin min man khalaqa tafdhwiila" Maana yake: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenipa afya mimi kwa hili alilompa mtihani huyu, na akanifanya kuwa bora kuliko wengi nakuwa miongoni mwa wale aliowaumba kwa ubora. Kaipokea Imamu Tirmidhiy

Swali: 42- Dua kwa mtu atakayehofia kukipa kijicho kitu.

Imekuja katika hadithi: "Atakapoona mmoja wenu kwa ndugu yake au kwake mwenyewe, au katika mali yake chenye kumstaajabisha, [Basi na akiombee baraka] kwani kijicho ni kweli (kipo)" Kaipokea Ahmadi na bin Maaja.

Swali: 43- Ni vipi unamtakia rehema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake?

"Allaahumma swalli 'alaa Muhammad wa a'laa aali Muhammad, kamaa swallaita 'alaa Ibraahiima wa 'alaa aali Ibrahiima, Innaka hamiidun majiid, Allaahumma baarik 'alaa Muhammad wa 'alaa aali Muhammad kamaa baarakta 'alaa Ibraahiima wa 'alaa aali Ibrahiima, Innaka hamiidun majiid" Maana yake: Ewe Allah shusha rehma juu ya Muhamad na ali zake (familia yake) Muhamad kama ulivyo shusha juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu, na shusha baraka juu ya Muhamad na watu wa Muhamad kama ulivyo shusha baraka juu ya Ibrahim na watu wa Ibrahim hakika wewe ni mwenye sifa tukufu. Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Sehemu ya maamrisho:21

Swali: 1- Ni zipi hukumu tano za kutekelezwa kisheria?

Jawabu:
1- Wajibu (Faradhi)
2- Sunna.
3- Haramu.
4- Machukizo (Makruhu).
5- Halali.

Swali: 2- Fafanua hizi hukumu tano.

Jawabu:
1- Wajibu (Faradhi): Mfano kama swala tano, na kufunga mwezi wa ramadhani, na kuwatendea wema wazazi wawili.
-Jambo la wajibu hulipwa thawabu mfanyaji wake ni huadhibiwa mwenye kuliacha.
2- Sunna: Mfano kama swala za sunna zenye mpangilio (Sunani Rawatibu) Na kisimamo cha usiku, na kulisha chakula, na kutoa salamu, na huitwa sunna au Mandubu.
-Jambo la Sunna hulipwa mfanyaji wake na wala haadhibiwi mwenye kuliacha.
Angalizo muhimu:

Ni lazima kwa kila muislamu anaposikia kuwa jambo hili ni sunna au linapendeza (Mandubu) afanye haraka kulitekeleza, na kumuiga Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.
3- Haramu: Mfano kunywa pombe na kuwaasi wazazi wawili, na kukata udugu.
-Haramu hulipwa mwenye kuiacha na huadhibiwa mwenye kuifanya.
4- Machukizo (Makruhu): Mfano kama kupokea na kutoa au kumpa mtu kwa mkono wa kushoto, na kufunua nguo ndani ya swala.
-Machukizo hupata malipo mwenye kuyaacha na wala haadhibiwi mwenye kuyafanya.
5- Halali: Mfano kama kula tufaa (Apple) na kunywa chai, na huitwa: yanayoruhusiwa au kwa jina jingine halali.
-Mambo ya halali hapati malipo mwenye kuyaacha na wala haadhibiwi mwenye kuyafanya.

Swali: 3- Ni ipi hukumu ya kuuza na miamala?

Jawabu: Asili katika biashara zote na miamala yote ni halali, isipokuwa baadhi ya aina ambazo kaziharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na amehalalisha Mwenyezi Mungu biashara na akaharamisha riba" [Suratul Baqara: 275].

Swali: 4- Eleza baadhi ya aina za miamala na biashara za haramu?

Jawabu:
1- Ghushi, na miongoni mwake: ni Kuficha aibu za bidhaa.
Na kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alipita katika gunia la chakula, akaingiza mkono wake ndani yake, vidole vyake vikapata unyevunyevu, akasema: "Ni nini hiki ewe muuza chakula?" Akasema: Kimenyeshewa na mvua ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema: "Kwa nini usikiweke juu ili watu wakione? Yeyote mwenye kudanganya si miongoni mwangu" Imepokelewa na Imamu Muslim
2- Riba: Na miongoni mwake, ni kuchukua deni la elfu moja kwa mtu ili nije kumlipa elfu mbili.
Na ziada ndio riba iliyoharamishwa.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na amehalalisha Mwenyezi Mungu biashara na akaharamisha riba" [Suratul Baqara: 275].
3- Udanganyifu na kutoeleweka: Kama kuuza maziwa yakiwa katika chuchu za mnyama, au kuuza samaki wakiwa majini kabla ya kuwavua.
Imekuja katika hadithi:
"Alikataza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake biashara ya udanganyifu" Imepokelewa na Imamu Muslim

Swali: 5- Taja baadhi ya neema za Mwenyezi Mungu juu yako.

Jawabu: 1- Neema ya uislamu, nakuwa wewe si katika watu wapingaji.
2- Neema ya mafundisho ya Mtume (Sunna), nakuwa wewe si miongoni mwa wazushi.
3- Neema ya uzima na afya, kama masikio na macho na kutembea na zinginezo.
4- Neema ya vyakula, vinywaji na mavazi.
Na neema zake Mtukufu juu yetu ni nyingi hazihesabiki wala hazidhibitiki kwa idadi maalumu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na mkijaribu kuzihesabu neema za Mwenyezi Mungu kwenu, ili mjue idadi yake, hamuwezi kuzidhibiti kwa wingi wake na utofauti wake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, ni Mwenye huruma kwenu, kwani Anasamehe kasoro zenu za kutotekeleza ushukuru wa neema, wala Hazikati kwenu, kwa kukiuka kwenu mipaka, wala Hawaharakishii mateso". [Suratun nahli: 18]

Swali: 6- Ni upi wajibu wetu katika neema? Na ni vipi utashukuru kwa neema ulizonazo?

Jawabu: La wajibu: Ni kushukuru, na kunakuwa kwa kumsifu Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa ulimi na yakwamba yeye pekee ndiye mwenye fadhila, na kwa kuzitumia neema hizi katika yale yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kwa kumuasi.

Swali: 7- Ni zipi sikukuu za waislamu?

Jawabu: Sikukuu za Fitri na Adh-ha (Iddil Fitri na Iddil Adh-ha)
Kama ilivyokuja katika hadithi ya Anasi, Amesema: Alikuja Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika mji wa Madina akakuta wakiwa na siku mbili ambazo wanazitumia kwa kucheza ndani yake, Akasema: "Ni za nini siku hizi mbili?", Wakasema: Tulikuwa tukicheza ndani yake zama za ujinga, akasema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amekubadilishieni kwa siku hizo mbili siku bora kuliko hizo: Sikukuu ya Adh-ha, na sikukuu ya Fitri" Kaipokea Abuudaud.
Sikukuu zingine zisizokuwa hizo basi hizo ni katika uzushi.

Swali: 8- Ni upi mwezi bora?

Jawabu: Mwezi wa ramadhani.

Swali: 9- Ni ipi siku bora?

Jawabu: Ni siku ya Ijumaa.

Swali: 10- Ni ipi siku bora katika mwaka?

Jawabu: Ni siku ya Arafa.

Swali: 11- Ni upi usiku bora katika mwaka?

Jawabu: Ni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri).

Swali: 12- Ni lipi la wajibu unapomuona mwanamke wa kando (asiyekuwa ndugu yako)?

Jawabu: La wajibu ni kuinamisha macho, Amesema Mtukufu: "Sema kuwaambia waumini wa kiume wainamishe macho yao" [Suratun Nuru: 30]

Swali: 13- Ni wapi maadui wa mwanadamu?

1- Ni nafsi yenye kuamrisha maovu: Nako ni mtu kufuata yale ambayo nafsi yake inamtuma na matamanio yake katika kumuasi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, Amesema Mtukufu: "Hakika nafsi huamrisha maovu mno, isipokuwa ile ambayo Mola wangu mlezi aliyoirehemu, Hakika Mola wangu Mlezi ni msamehevu na Mwenye kurehemu" [Suratu Yusuf: 53] 2- Shetani: Na huyu ni adui wa mwanadamu, na lengo lake ni kumpoteza na kumtia wasi wasi ili aingie katika shari na amuingize motoni. Amesema Mtukufu: "Na wala msifuate nyayo za shetani, hakika yeye kwenu nyinyi ni adui wa wazi". [Suratul Baqara: 168]. 3- Watu waovu: Wanaohamasisha katika shari, na wanazuia kheri. Amesema Mtukufu: "Marafiki katika kumuasi Mwenyezi Mungu duniani watatengana wao kwa wao Siku ya Kiyama. Lakini wale waliofanya urafiki juu ya uchaji Mwenyezi Mungu, urafiki wao utadumu duniani na Akhera". [Suratuz zukhruf: 67]

Swali: Toba ni nini?

Jawabu: Toba: Ni kurudi kutoka katika kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu kuja katika utiifu. Amesema Mtukufu: "Na mimi ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia kutokana na dhambi zake na ukanushaji wake, akaniamini mimi na akafanya matendo mema kisha akaongoka kufuata njia ya ukweli na akasimama imara juu yake." [Suratu Twaha: 82]

Swali: 15- Ni zipi sharti sahihi za kufanya toba?

Jawabu: 1- kujiondoa katika dhambi.
2- Kujuta kwa yaliyopita.
3- Kuazimia kutorudia kosa.
4- Kurudisha haki na mali za dhulma kwa wenye nazo.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na wale ambao wakitenda dhambi kubwa au wakizidhulumu nafsi zao kwa kutenda dhambi chini ya hizo, wanaikumbuka ahadi ya Mwenyezi Mungu ya malipo mema kwa wanaomtii na malipo mabaya kwa wanaomuasi na wanaelekea kwa Mola wao hali ya kutubia wakawa wanamuomba Awasamehe madhambi yao na wakawa wana yakini kwamba hapana anayesamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wao kwa sababu hiyo hawaendelei kwenye maasi, na wao wanajua kwamba wakitubia Mwenyezi Mungu Atawakubalia toba yao". [Surat Al Imran: 135]

Swali: 16- Nini maana ya kumtakia rehema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake.

Jawabu: Maana yake Yakwamba wewe unamuomba Mwenyezi Mungu ampe sifa nabii wake Rehema na Amani ziwe juu yake kwa walioko juu.

Swali: Nini maana ya Sub-haanallaah (Ametakasika Mwenyezi Mungu?

Jawabu: Ni tasbihi (kumtukuza Mwenyezi Mungu) nako ni kumtakasa yeye aliyetakasika na kutukuka kutokana na kila pungufu na aibu na ovu.

Swali: 18- Nini maana shukurani?

Jawabu: Ni kumsifia Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumsifu kwa kila sifa ya ukamilifu.

Swali: 19- Nini maana ya Allahu Akbaru? Mwenyezi Mungu Mkubwa?

Jawabu: Nikuwa yeye aliyetakasika ni Mkubwa kuliko kila kitu na mtukufu na ni muheshimiwa kuliko kila kitu.

Swali: 20- Nini maana ya Laa haula walaa quwwata illa billah (Hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu)?

Jawabu: Hakuna ujanja kwa mja wa kutoka hali moja kwenda hali nyingine, na wala hana nguvu juu ya hilo isipokuwa kwa nguvu za Mwenyezi Mungu.

Swali: 21- Nini maana ya Astaghfirullaah (Ninamuomba msamaha Mwenyezi Mungu)?

Jawabu: Yaani: Ni mja kuomba kutoka kwa Mola wake ayafute madhambi yake, na azisitiri aibu zake.